ARUSHA.
Waziri wa Elimu ,Mafunzo na Ufundi Profesa
Joyce Ndalichako akiwasili katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson
Mandela ambapo amezindua mradi wa Vituo vya Umahiri utafiti wa kilimo na
Magonjwa ya binadamu pamoja na mradi wa kuongeza ujuzi kwa kazi za uzalishaji
zinazoleta tija uliofadhiliwa na Benki ya Dunia.
PHOTO: Waziri wa elimu, sayansi, teknolojia na ufundi Profesa, Joyce
Ndalichako (wa pili kushoto) akisikiliza maelezo juu ya uendeshaji na namna mradi utakavyoendeshwa.
|
HABARI KWA UNDANI.
Benki ya Dunia imetoa kiasi cha fedha cha
Dola Milioni 120 ambazo ni sawa na Bilioni 200 za kitanzania ili kuwezesha
miradi ya elimu na ujuzi kwa ajili ya kazi zinazoleta uzalishaji wenye tija
pamoja na vituo viwili vya umahiri vya kikanda.
Akizungumza katika uzinduzi wa Miradi hiyo
Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa miradi hiyo
itasaidia kuongeza watu wenye ujuzi wa kati ambao watafanya kazi katika sekta
za kilimo, Utalii, Ujenzi, nishati na madini.
"huu ni moja ya miradi iliyofadhiliwa pamoja
na vituo vingine vya umahiri katika masuala ya utafiti wa kilimo na magonjwa ya
binadamu ikiwemo viwili vinavyomilikiwa na Chuo kikuu cha Nelson Mandela pamoja na vituo
vingine viwili vilivyopo katika Chuo cha Kilimo cha Sokoine University of
Agriculture" alisema Prof. Ndalichako.
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za
Tanzania,Malawi, Burundi na Somalia Bella Birds alisemaa kuwa uboreshwaji wa
rasilimali watu kwa kuongeza ujuzi uliokosekana utasaidia taifa kufikia malengo
yake ya kufikia uchumi wa viwanda.
"inakadiriwa kuwa Vijana
milioni 1 huitimu katika vyuo mbalimbali na kuingia katika soko la ajira kila mwaka hivyo inatarajiwa kuwa nafasi za ajira kwa vijana hao zitatengenezwa na sekta binafsi
iwapo zitashirikiana vyema na serikali husika" alisema Bella Birds.
Wakati huo huo makamu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha
Nelson Mandela Karoli Njau alisema kuwa mradi huo utasimamiwa kwa makini ili
kuhakikisha kuwa malengo yanafikiwa hususan katika vituo vya umahiri pamoja na
mradi wa ujuzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania (TPSF) Godfrey Simbeye amesema kuwa kulikua na upungufu
mkubwa wa watu wenye ujuzi nchini kutokukidhi mahitaji ya soko la ajira hivyo
kulazimu waajiri kuajiri watu kutoka nje jambo linalogharimu fedha nyingi hivyo
mradi huo utasaidia vijana 30,000 kupata ujuzi utakaokidhi mahitaji ya soko la
ajira.
Post a Comment