ARUSHA.
Wabunge
wa baraza la wawakilishi pamoja na wafanyakazi wa balaza la wawakilishi wamefanya zira ya ujirani mwema wakiwemo wanamichezo
kutoka afisi ya balaza la wawakilishi Zanzibar jijini Arusha ikiwa ni katika mapumziko ya
shughuli za Bunge.
Katka ziara hiyo iliyowapeleka
kutembelea baadhi ya vivutio vya utalii mkoani Arusha wabunge hao wakiongozwa
na spika la balaza la wawakilishi Zubeir Ally Maurid pamoja na Mwenyekiti wa balaza Hamad Matary waliweza
kufanya utalii wa ndani pamoja na michezo mbalimbali, ikiwemo ya kukimbia kwa
magunia, kukimbia 100mita, mpira wa miguu, mpira wa mikono kwa wanawake, pamoja
na michezo mingine mbalimbali.
Hizi hapa chini ni
picha chache za matukio mbalimbali zinazohusisha ziara na michezo kadhaa
iliyochezwa katika kiwanja cha General Tire jiji Arusha.
PHOTO: Kushoto ni mbunge (jina halikupatikana) na wengine ni Watumishi
wa balaza la wawakilishi Zanzibar na kutoka ofisi ya wazee wa Arusha wakikimbia
wakiwa ndani ya magunia.
|
PHOTO: Huu ni mchezo wa kukimbia huku ukiwa na kijiko mdomoni chenye limau juu yake...
|
PHOTO: Hapa wakicheza mashindano ya kufukuza kuku.
|
PHOTO: Wachezaji wa mpira wa mikono kwa
wanawake (Netball) wakicheza mashindano ya ujirani mwema.
|
Post a Comment