Mzee huyo
anayejulikana kwa jina Kofi Asilenu mwenye umri wa miaka 80 ambaye ni baba wa
watoto 100 na wake 12, anaishi na familia yake katika kijiji chaAmankrom
kilicho umbali wa kilomita 45 kutoka mji mkuu Acca.
Familia yake ni theluthi moja ya watu 600
katika kijiji hicho, amesema kuwa anataka familia kubwa kwa sababu hakuwahi kuwa na ndugu. “Sina kaka wala shangazi, ndiyo sababu niliamua
kuwa na watoto wengi ili wapate kunipa maziko yaliyo mazuri siku nikifa” alisema
Kofi.
Hata hivyo hiyo familia yake inamgharimu kwa
sehemu kubwa. anasema alikuwa mtu mwenye mali, lakini mali hiyo ilipungua
kutokana na gharama ya kuitunza familia yake kubwa
Kofi Asilenu
anaonekama kuwa mwenye afya nzuri na hata anasema ana nia ya kuwa na watoto zaidi ya hao.
Post a Comment