Mwanaume kutoka nje ya ndoa haijamanisha kama hampendi mkewe!, na 95% ya wanaume wenye mausiano wanaiba au kuchepuka kidogo.
Siku moja dada yangu alimfumania mmewe akaamua kurudi nyumbani kwetu, kabla hajaingia ndani Mama akamuuliza, kulikoni? Dada akaanza kueleza Huku akitoa machozi. Khakushangaza Mama Hakumuruhusu dada kuingia ndani kama alivyokua akitarajia kupata faraja kutoka kwa mama yake.
Alimwambia Sasa hivi wewe ni mke wa mtu, hapa nyumbani tumeshakutoa katika hesabu, cha msingi msamehe mmeo na urudi kwako haraka kabla hiyo michepuko haijaingia ndan kwako.
Dada aliongenza kilio na alikua Anatia huruma sana na mama alizidi kumkazia Macho nakumtaka arudi haraka iwezekanavyo. Nakumbuka ilikua mida ya mlo wa mchana na Chakula kilikua tayari ila hakuruhusiwa hata kula.
Alichopewa ni pesa ya taxi ya kumrudisha kwake huku akiambiwa awahi kumpikia mmewe, alicho mshauri ni kwamba kama mmeo analewa sana na hakuachii Pesa ya matumizi na anaporudi anakupiga sana hapo nitakupokea hata mahari tutarudisha, Ila kama ni kuhusu michepuko naomba urudi kwako haraka Sana.
Siku hiyo nilidhani kama sio mama yetu, ila baada ya dada kuondoka nilimuuliza mama kwa nini hakumpa nafasi dada hata atue mizigo yake au akae hata siku moja?! Ndipo mama akaanza kunisimlia mambo mengi kuhusu Mzee (Baba) na kuhusu wanaume.
Moja kati ya mambo hayo ni kuhusu mtoto wa jirani yetu ni mdogo wangu ambae mzee kazaa nje na bado Mama alimsamehe Mzee Na Wmwakaendelea na maisha na leo wanalea wajukuu....!
Mpaka leo hii sijasikia dada anakuja nyumbani kutoa Malalamiko au kusema chochote kuhusu ndoa yake....!
Ushauri wangu kwako wewe unaesoma Slstory hii, usiombe hama usiwe na haraka kuomba ushauri kwa mtu yeyote yule kuhusu NDOA au mahusiano yako, hata kama ni mama yako.
Jaribu kukaa na mwenzio myamalize kwani katika kila Ndoa Kuna DOA hivyo huenda unaemwadisia akawa Na DOA kubwa kuzidi lako, pili hujui unayemuhadithia ana nia gani Na Wewe.
Nimesema hata kama ni mama yako.
Lakini tatu, bila uvumilivu huwezi kuishi na mtu yeyote, hivyo basi unatakiwa kuilinda na kuitunza Ndoa yako au uhusiano wako, na mwisho mtangulize MUNGU katika yote na utadumu milele katika NDOA yako.
Story from Leo Kilangi.
Post a Comment