PHOTO: Mwanafunzi aliyejulikana kwa jina la
Neema aliyelala chini akifanyiwa maombi na wanafunzi wenzake.
|
PHOTO: Mmojawapo wa wanafunzi (kushoto) waliojitolea
akiwa na mwalimu wake (kulia) wakimuombea mwanafunzi aliyeshikwa na mapepo
wakiwa darasani kwenye masomo.
|
PHOTO: Wanafunzi na Walimu wakiwa kwenye makundi
tofauti wakiwaombea baadhi ya wanafunzi waliopatwa na mapepo.
|
PHOTO: Aliyekaa ni mmoja wa wanafunzi
aliyepata nafuu
mara baada ya maombi, akifarijiwa na mwenzake.
|
MTWARA.
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida wanafunzi wanaosoma kwenye Chuo cha elimu ya ufundi na tasnia ya Hotel VETA kilichopo pembezoni
mwa bahari ya Hindi mkoani Mtawara, walipatwa na hali iliyosemekana kuwa ni
mapepo na kuanza kupiga kelele huku baadhi ya wanafunzi wenzao wakipatwa na
wasiwasi kutojua nini wafanye.
Wakati
hali hiyo ikijitokeza na kupelekea wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza kusitisha
masomo yao kwa siku ya leo, iliwafanya baadhi ya wanafunzi na walimu kufanya
maombi na kuanza kukemea mapepo hayo ambapo baadhi ya wanafunzi walionekana
kutokuwa na Imani na kutaka kukimbia wakiogopa kupata dhoruba kutoka kwa madudu
hayo.
Mmoja
wa Walimu anayefundisha wanafunzi walipatwa na dhahama hiyo Mwalimu Christina Masalu
anayefundisha masomo ya Ukarimu/Hospitality anasema wanafunzi walianza
kudondoka darasani akiwa anafundisha ambapo katika tukio la leo ilimpa mshtuko
kutokana na kuwa si mara ya kwanza, kwa mara ya tatu hii mimi binafsi imenipa
mshtuko na imenipa shida kidogo, hali iliyonipelekea kukaa na wanafunzi na
kuwauliza tufanye nini…”
Mkuu
wa chuo hicho aliyejulikana kwa jina moja Kibeherehakuweza kuzungumzia hali
hiyo kutokana na tukio hilo na ameahidi kufuatilia na kujua kilichotokea ambapo
atatoa taarifa hapo baadaye.
>>Habari kwa undani juu ya tukio hili angalia kupitia Habari Video
muda mfupi ujao pia tembela You Tube Chanel yetu ya TODAYS NEWS.
Post a Comment