0
PHOTO: Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda
 (katikati) akifunga mafunzo elekezi, kushoto kwake
 ni muwezeshaji Shimbona kulia ni mkuu wa
wilaya ya Newala. 
MTWARA
Mafunzo elekezi ya siku mbili yaliyowashirikisha madiwani, mameya, wenyeviti wa wilaya,  wakurugenzi, wakuu wa wilaya na maofisa wa serikali kutoka mkoa wa Mtwara yamefungwa jana jioni na  Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda Herman 

Katika hotuba yake ya kufunga amesema mafunzo hayo yatakuwa na tija endapo wahitimu watafanyia kazi kutokana na juhudi za wawezeshaji na mafunzo waliyotoa,  pia kwa upande wa rushwa amesema, 

"ikiwa hutaichukia rushwa huwezi kuizuia, hivyonkutokana mafunzi haya tunategemea rushwa itakomeshwa si kwa kutumia nguvu ila kutokana na mafunzo haya basi tutakuwa na ya kuweza kuzuia".

Pia amesema jambo la ushirikishwaji wa wananchi katika maendeleo ni jambo la msingi maana maendeleo yanawahusu wananchi moja kwa moja. 

"naunga mkono utolewaji wa mafunzo haya kwa mara nyingi ili watu wasisahau,  lakini pia mtoto anapoenda darasani anaenda kuoewa elimu bila malipo,  ila mtu mzima anapoenda kusoma analipwa pia hii nikutokana na mazingira ya elimu inayotolewa". Alisema DC Mmanda. 

Aitha amezitaka serikali za mitaa kukusanya mapato ili kuweza kuwa na uwezi wa mapato na kuweza kuwa na nafasi ya kutoa elimu kwa viongozi wake pale inapobidi, mwani serikali ya mtaa ni daraja kati 

PHOTO: viongozi na watumishi waliohudhulia mafunzo wakifuatilia hotu a ya kuhitimisha mafunzo kutoka kwa Mkuu wa wilaya (pichani juu) 

Wakati huo huo mmoja wa wawezeshaji anayetoa mafunzo aliyefahamika kwa jina la Shimba amewataka madiwani hao kutoka wilaya zote za mkoa wa Mtwara kuhakikisha wanayafanyia kazi mafunzo waliyopewa na wakufunzi kutoka chuo cha taifa kinachotoa mafunzo ya utumishi wa Umma cha Homboro, 

Kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo hayo mmoja wa madiwani ambaye alikuwa mwenyekiti (jina halikuweza kupatikana) amesema wao kama viongozi katika jamii wataenda kuyafanyia kazi lakini watakuwa tayari kwa wakati mwingine kuhudhulia mafunzo hayo ikiwa na maana Elimu haina mwisho na ellimu hii kufikia miaka ya mbeleni haitakuwa hii tena,  bali kutakuwa na mapya zaidi ya leo,  "tunaomba mtuletee mafunzo kama haya wakati mwingine jana na leo isiwe mwisho".

Katika mafunzo hayo yanayofadhiliwa na USAID ikiwa ni msaada kutoka kwa watu wa Marekani yamegusia nyanja ya Rushwa ikiwa ni pamoja na kwenye mifumo kwa sekta zote,  pia  yamegusia sehemu ambazo viongozi hao watakuwa karibu na maeneo husika ya kiutendaji.

Post a Comment

 
Top