0

DODOMA.
Chama cha mapinduzi (CCM) mkoani Dodoma kimefanya mkutano/semina kwa viongozi ambao ni makatibu kata wa kata zote za Dodoma mjini ikiwa ni lengo mahususi kuwajengea uwezo na kuwaweka tayari kwa uchaguzi wa chama hicho kuanzia na kata, pamoja na kuwawezesha viongozi kuwaruhusu wananchama kuchukua fomu bila ubaguzi na upendeleo.


PHOTO: Katibu wa CCM wilaya ya Dodoma mjiji Pili Augustino akiongea wakati wa kuwatambulisha viongozi wa kata kwa mgeni rasmi katika semina ya wanachama kufanya uchaguzi na kuchukua fomu na kuwawezesha makatibu kata.

PHOTO: Katibu wa ccm mkoa wa Dodoma Jamila Yusuph (kushoto) akipokea mchango wa shilingi 500,000 kutoka kwa katibu wa siasa na uhusiano Ngemela Lubinga.

PHOTO: Baadhi makatibu kata wa chama cha mapinduzi wa Dodoma mjini waliohudhulia mkutano/semina elekekezi kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa ccm kwenye kata mkoa wa Dodoma.

PHOTOKatibu wa siasa na Uhusiano na mjumbe wa NEC Ngemela Lubinga akiongea wakati wa kufungua semina na kuwaeleza viongozi wa kata za Dodoma mjini kuhusu uchaguzi na makusudi ya chama kufanya mabadiriko.

PHOTO: Wanachama, viongozi, makatibu kata wa ccm dodoma mjini  waliohudhulia semina elekezi iliyofanyika makao makuu ya ccm Dodoma, wakimsikiliza katibu wa siasa na uhusiano (hayupo pichani) .

PHOTO: Katibu wa siasa na Uhusiano na mjumbe wa NEC Ngemela Lubinga (aliyesimama kulia) akiongea wakati wa kufungua semina na kuwaeleza viongozi wa kata za Dodoma mjini kuhusu uchaguzi na makusudi ya chama kufanya mabadiriko.

PHOTO: Katibu wa ccm mkoa wa Dodoma Jamila Yusuph (alishika pesa) alizopokea kutoka ka Katibu wa siasa na uhusiano Ngemela Lubinga mwenye miwani, wengine wanaoshuhudia (kulia) Pili Augustino (wa kwanza kulia) (wa pili kutoka kulia) 



Akifungua semina hiyo iliyojumuhisha makatibu kata na viongozi kadhaa wa chama hicho katika ofisi za CCM makao makuu Dodoma, Katibu wa siasa na Uhusiano ndani na nje ambaye pia ni mjumbe wa halmashauli kuu ya CCM taifa Ngemela Lubinga kwanza aliwataka viongozi hao na wanachama kusimama kwa dakika mbili ili kuwakumbuka wanafunzi 32 pamoja na walimu na dereva wao waliofariki dunia katika ajali mkoani Arusha.

Amesema wanachama na viongozi wa wanachama wa ccm wanapaswa kuwaelimisha wengine kwani yawezekana bado hawaekielewi vizuri chama cha mapinduzi kwa sababu ya kutokuwa na elimu ya kutosha, kwani hata mafanikio yaliyopatikana kutokana na uchaguzi uliopita kwa wilaya ya Dodoma mjini kufanya vizuri, siyo wana ccm tu waliotupa kura hata wasio wana ccm.

“Hayati mwalimu Nyerere alipolala akaota kuhamishia makao makuu ya nchi Dodoma alijua kuwa ninyi mnajua nchi hii inataka na inafanya nini, kwa sababu hivi vitu haviji hivihivi tu hata wazee wetu hawa wa zamani wanaelewa kuwa hakuna mtu aliyemshawishi Mwalimu Nyerere ahamishie makao makuu hapa” Alisema Comrade Lubinga.

Aitha amewataka viongozi na wanachama hao kuondokana na mazoea ya zamani ambayo waliyazoea kwani kwa sasa chama kinayafanya marekebisho makubwa kimfumo na hali hiyo inaweza kuleta kutoeleweka kwa baadhi ya wanachama.

Amewataka viongozi waliopewa dhamana kuacha kulialia bali wawajibike kama Baba au Mama anavyowajibika katika familia, pia amesema viongozi wanaofanya kazi kwa mazoea na kutofanya majukumu yao watachukulia hatua kutokana na kutafuata utaratibu katika nafasi zao.

Katika taarifa ya uchaguzi iliyosomwa na katibu wa ccm wilaya ya Dodoma mjini Pili Augustino amesema uchaguzi unaendelea katika mashina na kata ambazo hazijafanya uchaguzi huku akiwataka wanachama kuchangamkia fomu.


Ameendelea kusema “Chama kinaendelea kusimamia jumuiya zake ili ziweze kufanya uchaguzi ili kuendana na ratiba iliyopangwa, pia madarasa, makambi ya wanachama yarejeshwe kwa ngazi zote ili kuwafundisha wanachama wetu katika misingi ya uwajibikaji na uzalendo”.




Post a Comment

 
Top