Maelfu ya wananchi wa mkoa wa Arusha na wengine kutoka mikoa ya
jirani leo walijitokeza kwa wingi kuhudhuria ibada ya pamoja kuwaaga wanafunzi
32 wa shule ya Lucky Vicent waliofariki dunia ajali katika eneo la Rhotia Merera, wilaya ya Karatu siku ya jumamosi asubuhi walipokuwa safarini kwenda kufanya mtihani wa ujirani mwema.
PHOTO: Mmoja wa waombolezaji akifarijiwa na wananchi waliofika katika uwanja wa sheikh Amri Abeid kuhudhulia ibada ya kuwaaga wanafunzi, walimu na dereva waliofariki kutoka na ajali. |
--------------------------------------------------------------------------------------
|
PHOTO: Katika
hali kama hii uwezi kujizuia kutokana na majonzi hama huzuni inayoweza
kujitokeza, hapa mmoja wa waombolezaji alizirai na kupewa huduma ya kwanza.
|
SHORT BRIEFING:
ARUSHA.
Katika ibada hiyo majeneza 35 yenye miili ya wanafunzi,
walimu wawili na dereva aliyekuwa akiendesha basi dogo yalifikishwa katika
uwanja wa Sheikh Amri Abeid, kwa ibada ya mwisho ya kuwaaga kabla ya kufanyika
mazishi sehemu tofauti.
Katika hali ya kuonyesha huzuni na majonzi shughuli nyingi
katika jiji la Arusha zilisimama tangu mapema na hata maduka na
biasharanyingine zilifungwa huku watu wengi wakielekea uwanjani kuhudhuria ibada
hiyo.
Aitha katika huduma hiyo ya ibada ya jumla Kiongozi mkuu wa
serikali aliyehudhulia alikuwa ni makamu wa Rais Bi Samia Suluhu Hassan ambaye
alikuwa miongoni mwa viongozi wakuu waliohudhuria ibada hiyo, ambapo katibu
mkuu wa CCM Abdulrahman kinana pia alihudhulia ibada hiyo na kwa niaba ya chama
alitoa pole kwa wafiwa na watanzania.
Katika salamu za rambirambi na kulihutubia taifa makamu wa
Rais Bi Samia amevitaka vyombo husika likiwemo jeshi la polisi kuhakikishe
suala la usalama barabarani linapewa kipaumbele. "Nawaasa madereva kuwa makini wawapo
barabarani na serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya barabara," amesema.
Kwa upande mwingine Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye juzi
alilazimika katika hotuba yake kuwaomba viongozi kusimama kwa dakika moja
kuwaobea dua marehemu, leo aliwakilishwa na waziri wa elimu wa Kenya Dkt Fred
Matiang'I, ambaye alikuwa mmoja wa wageni kutoka nje ya Tanzania waliohudhuria
ibada hiyo, ambapo amewapa pole Watanzania kwa msiba huo.
"Kenya
itaendelea kuwa pamoja nanyi kwenye kipindi hiki kigumu cha msiba huu mzito
uliowafika, msiba huu si wa Tanzania peke yake ni wa wote hata kwetu Kenya Rais
Kenyatta na mkewe wanawapa pole sana na kuwaombea," amesema.
Naye Rais Magufuli kupitia ujumbe kwenye Twitter, ameelezea,
jinsi alivyopatwa na huzuni kutokana na ajali hiyo.alisema "Nimepatwa na uchungu na majonzi
makubwa ninapoyaona majeneza ya watoto na walezi wao waliopoteza maisha katika
ajali ya basi huko Arusha. Tumewapoteza mashujaa wetu katika elimu,"
Rais Magufuli, akituma salamu za rambirambi Jumamosi
alisema, ajali hiyo imezima ndoto za watoto waliokuwa wakijiandaa kulitumikia
taifa na imesababisha uchungu, huzuni na masikitiko makubwa kwa familia za
marehemu na Taifa kwa ujumla."
"Muhimu
kwa sasa tuwaombee marehemu wote wapumzishwe mahali pema, majeruhi wapone
haraka na wote walioguswa na msiba huu wawe na moyo wa subira, ustahimilivu na
uvumilivu katika kipindi hiki kigumu."
Kwa upande mwingine wabunge
wamekubali kukatwa posho za siku mbili kwa ajili ya kutoa rambirambi kwa wazazi
wa watoto hao, ambapo kwa siku mbunge hulipwa Sh 220,000 kama posho ya kikao
kimoja, pia makampuni mengine yaliyochanga ni, Kampuni ya Ngorongoro wametoa 15mil,
Tanapa 20mil, AICC 5mil, Jiji la Arusha 5mil na Auwasa 1mil.
Pia
kulikuwa na wawakilishi wa Walimu 30 toka serikali ya mapinduzi Zanzibar katika
maombolezo hayo na vikosi vyote vya usalama likiwemo jeshi la Magereza, jeshi
la wananchi na Polisi walishiriki katika maombolezo hayo.
Source: lBBC
Post a Comment