PHOTO: Picha hii juu ni jumla ya wanafunzi, walimu wao na dereva waliofariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita. |
WALIOBAKI. |
PHOTO: Hizi hapa chini ni picha chache za tukio la Ajali iliyowaondoa wanafunzi wapatao 31 wakiwemo walimu na dereva wa basi walilokuwa wakisafilia.
ARUSHA.
Wanafunzi wapatao 31
wamefariki dunia katika ajali ya basi walilokuwa wakisafilia kutoka shuleni
kwao katika shule ya Luck Vicent ya jijini Arusha wakielekea katika wilaya ya
karatu kufanya mtihani wa ujirani mwema na wenzao wa shule tofauti.
Katika taarifa zilizopatikana mapema zinasema kuwa basi hilo aina ya mistubish Rosa lililokuwa
limewabeba wanafunzi hao lilikuwa katika mwendo wa kawaida na mkuu wa wilaya ya
Karatu amethibisha kutokea kwa ajali hiyo na akiwa katika eneo la tukio aliweza
kusema ataongea baadaye kwa undani.
Naye kamanda wa Polisi
mkoa wa Arusha Charles Mkumbo ambaye alithibisha kutokea kwa ajali hiyo amesema
wanafunzi waliofariki ni wa shule ya Luck Vicent ya jijini Arusha na wakati
akitoa taarifa hizi alikuwa njiani kuelekea eneo la tukio.
>>TODAYS NEWS: Msiba huu unamgusa kila mtu bali Mungu awape Nguvu na uvumilivu ndugu, jamaa na wote waliofikwa na msiba huu.
** Angalia kilichojili wakati wa ibada ya pamoja katika uwanja wa sheikh amri abeid katika ukurasa unafuata.
Post a Comment