0
DODOMA.

Mkutano mkuu wa mwaka wa Bodi ya korosho unafanyika makao makuu ya nchi mkoani Dodoma ikiwa ni maara ya kwanza kufanyika mkoani hapa, ambapo ujumbe rasmi  wa mwaka kwenye mkutano huo ni Korosho Dhahabu  ya Kijani.



PHOTO: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Viongozi wa Bodi ya Korosho alipowasili kufungua mkutano wa bodi ya Korosho, (katikati mwenye kiremba) Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho nchini Mama Anna Abdallah. 

PHOTO: Mbunge Mtama Nape (kushoto) oNnauye akibadirishaji mawazo na  viongozi mbalimbali wa serikali waliofika katika mkutano.

PHOTO: Mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Dodoma ambaye ni mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabrill Shekimweli akiongea wakati wa kufungua mkutano kwa kumwakilisha mkuu wa Mkoa.

PHOTO: Wakuu wa mikoa na Wilaya wanaotoka kwenye mikoa inayolima zao la korosho ukiwemo mkoa wa Njombe ambaye mkuu wake wa Mkoa Christopher Ole Sendeka (wa pili kutoka kushoto)

PHOTO: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kufungua mkutano wa Mwaka wa Bodi ya korosho unaofanyika katika katika Chuo cha Mipango na Maendeleo vijijini mjini Dodoma.

PHOTO: Wabunge wanaowakilisha mikoa ya kusini mwa Tanzania waliofika kuhudhulia mkutano wa mwaka wa Bodi ya korosho nchini.

PHOTO: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma hotuba (kushoto kwake) ni viongozi wa Bodi ya korosho pamoja na mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Dodoma, wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu  katika Chuo cha Mipango na Maendeleo vijijini mjini Dodoma.

PHOTO: Baadhi ya wakulima, Viongozi wa vyama, wanunuzi, wabanguaji waliohudhulia mkutano mjini Dodoma, wakifuatilia hotuba.



HABARI KWA UNDANI
Akifungua mkutano huo Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa amewataka wakulima wa zao hilo nchi kujikita katika uzalishaji wa korosho bora huku akiwataka kuachana na mfumo wa kuuza korosho nje  ya soko lisilokubalika badala ya kuuza kupitia  vyama vya ushirika, hama kwa wanunuzi wanaotambulika.


Pia amepiga marufuku wanunuzi wa korosho kwa njia za panya ambao wamekuwa wakipeleka zao hilo nje ya mipaka ya nchi pasipo vibali au kununua nje ya soko lisilotambulika ikiwa ni pamoja na kuwarubuni wakulima kuuza nje ya nchi au kwa magendo na kwa njia ya panya, “Nawaonya wanunuzi wa korosho nchini kuwa makini na tabia ya kwenda kwa wanunuzi wa korosho nje ya nchi na kuwarubuni au kuwadanganya ili wasije nchini kununua korosho, tukikutambua tutakufa na wewe.

Vile vile waziri mkuu amevitaka vyombo vinavyohusika na utoaji wa mikopo kama mabenki kuangalia namna mpya itakayoweza kuwafanya wakulima wa korosho kuweza kupata fedha/mikopo kwa wakati ili wakulima waweze kununua pembejeo muhimu kwenye matumizi ya shambani na hata inapobidi wakati wa kuvuna. 

Wakati huohuo mikoa kadhaa hapa nchini kama Tabora, Pwani, Dodoma, Singida na imeanza kulima zao hilo ambalo serikali kupitia Waziri wa kilimo na mifugo Dr. Charles Tizeba wameahidi kuwasaidia wakulima kupata masoko ya uhakika huku Waziri wa kilimo akitoa nafasi kwa wakulima kupata mbolea na pembejeo muhimu bure. 


Mkutano huo unaotazamiwa kumalizika leo unamalizika huku wajumbe wakitarajia kuondoka na maazimio yenye lengo la kunyanyua zao hilo huku mikoa mingine nchini ambayo haikuwa inalima zao hilo ikipewa kipaumbele kuanza kupanda zao hilo. 
             On Progress ....




Post a Comment

 
Top