0
DODOMA.
Chama cha Mapinduzi CCM kinaendelea na mchakato wa kukijenga chama kutoka katika mfumo uliokifanya chama kuonekana kikiwa kwa ni kwa ajili ya baadhi ya wanachama, ambapo maandalizi na uchaguzi  kuanzia ngazi ya shina ukiwa umeanza kwa viongozi kutaka wanachama wapewe nafasi ya kuchukua fomu pasi upendeleo.

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogoro amefanya ziara mkoani Dodoma akitembelea mkoa wa Dodoma ikiwa ni moja baada ya mikoa 23 ambayo mpaka sasa ametembelea ambapo mkoani Dodoma ametembela ofisi ya Mkoa na baadaye kwenye miradi ya Uchumi  ya mkoa akiwa ameongozana na Katibu mkuu wa Uchumi na fedha Dr. Haule na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Kimbisa.

Katika mkutano na wanachama, viongozi wa ccm amewataka kuwa jasiri kutokana na ndiyo chama kinachoshika dora, pia amezungumzia malengo makubwa ya Chama pamoja na Serikali katika kuijenga Tanzania mpya na kutekeleza ajenda ya kuhamishia makao makuu ya nchi mjini Dodoma hatua ambayo mpaka sasa inaendelea vizuri.


Mabalozi kupimwa kulingana na Idadi ya wanachama.
Kufuatia mkutano huo, Nibu katibu mkuu amewataka mabalozi wa ccm nchini kote kufanya kazi ya kukijenga chama na siyo mjumbe kuwa na wanachama 20 bado anapewa nafasi ya kuwa mjumbe wa shina.

Ameongeza kuwa chama cha Mapinduzi kitafanya kazi na mjumbe wa shina mwenye kuwa na wanachama zaidi ya 100 huyo anaoneka kuwa ni mjumbe mwenye tija kwa chama, pia baadhi ya wanachama waosababisha wenzao kukichukia chama na wengine kuondoka katika chama basi huu ni wakati wa kufanya mbadiriko ndani ya nafsi ili uwe kila mtu awe mpya.

“Tunahitaji kufanya mabadiriko, tumeumizwa vya kutosha, tumeumizana vya kutosha, tumewazurumu wenzetu haki zao za msingi, sasa mwenyezi Mungu atusaidie tufanye mabadiriko ndani ya nafsi zetu ataka viongozi wa ccm mpya wawe ni nuru ili CCM Mpya na Tanzania Mpya ionekane”

>>Hapa chini ni picha tofauti 24 za matukio tofauti toka alipofika mpaka kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi kuu ambapo aliweza kuongea na wanachama na viongozi wa CCM mkoa wa Dodoma.


PHOTO JUU: Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Rodrick Mpogoro alipowasili katika ofisi za ccm mkoa wa Dodoma,
>> Akivishwa skafu na vijana wa chama alipowasili katika ofisi hizo.

PHOTO: Naibu Katibu Mkuu wa ccm Bara Mpogoro akisalimiana na viongozi waliompokea kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Dodoma.

PHOTO: Kulia ni Katibu mkuu wa Uchumi na fedha wa ccm Dr. Haule, (katikati)  Naibu katibu mkuu ccm Bara Mpogoro wakiweka sahihi katika kitabu cha wageni, kulia ni Mbunge wa EALA Adam Kimbisa.

PHOTO: Naibu Katibu CCM Bara Rodrick Mpogoro akiwaeleza jambo viongozi wa ccm katika ofisi za ccm mkoa wa dodoma.



PHOTO: Picha 7 zifuatazo hapa chini zinaonyesha ziara ya Naibu katibu mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogoro alipotembelea miradi kadhaa ya uchumi ya CCM Mkoa wa Dodoma, akiwa na Mkurugenzi wa fedha wa chama Dr. Haule, Mbunge wa EALA Kimbisa na viongozi wengine wa Mkoa.







PHOTO: Mara baada ya kutembelea miradi ya chama, kuwasili katika ukumbi wa mikutano wa makao makuu ya CCM, Walipokelewa na nyimbo kutoka kwa wanachama na viongozi mbalimbali.

PHOTO: Mmoja wa wanachama na Kiongozi wa ccm ambaye amefurahia jambo kutokana mapokezi ya Katibu mkuu ccm Bara alipowasili kwa ajili ya kuongea na wanaccm wa Dodoma.

PHOTO: Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma Jamila akiwakaribisha viongozi na kuelezea itihali ya mkutano kwa viongozi waliofika katika mkutano huo.

PHOTO: Mbunge wa Bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki Adam Kimbisa akiongea na wanachama wa ccm katika ukumbi wa mikutano wa ccm mjini Dodoma.


PHOTO: Baadhi ya wazee wa ccm na viongozi wa dini  waliofika kumsikiliza Naibu Katibu Mkuu CCM Bara.

PHOTO:  Naibu katibu mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogoro akiongea na wanaccm (hawapo pichani) na kuwaeleza malengo ya chama na kuwataka kuungana kutoka katika mazoea ya zamani.

PHOTO: Sehemu ya wanaccm na viongozi kutoka jumuiya mbalimbali za mkoa wa Dodoma.

PHOTO: Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi mkoani Dodoma wakimsikiliza Naibu katibu mkuu (hayupo pichani) katika ukumbi wa mikutano makao makuu ya ccm.

PHOTO: Chini pia ni viongozi na wanaccm wa mkoa wa Dodoma wakisikiliza kile kinazungumzwa na viongozi.



PHOTO: Hawa ni baadhi ya kinamama wanachama, viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama cha mapinduzi mkoa wa Dodoma wakifuatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu CCM Bara.

PHOTO: Baadhi ya wanachama wa ccm mkoa wa Dodoma waliohudhulia mkutano.





PHOTO's: TNEWS Correspondence in Dodoma.

Post a Comment

 
Top