0




DODOMA.
Taasisi isiyokuwa ya kiserikali inayofanya utafiti kwatika nyanja mbalimbali za kijamii na kuishirikisha jamii katika utafiti hapa nchini  TWAWEZA imetoa utafiti unaoonyesha muelekeo miongoni mwa watoto wenye umri wa miaka 9 mpaka 13 wengi wao hawawezi kufanya majaribio ya kiwango cha darasa la pili (Std 2).

Katika utafiti uliofanyika katika mikoa kadhaa inaonyesha asilimia 42 ya watoto kutoka kaya kasikini walifaulu majaribio ukilinganisha na asilimia 58 kutoka kaya tajili, hali hizi zinaonyesha kuwa mahali anaposhi mwanafunzi panachangia kwa kiasi kikubwa katika matokeo ya kujifunza kuliko hali ya kiuchumi na vitu vingine ambavyo uhusika katika kuleta Elimu.

PROFILE PHOTO: Mkurugenzi TWAWEZA Aidan Eyekuze.
Mkurugenzi mkuu wa TWAWEZA Aidan Eyekuze anasema “inatia moyo kuona watoto wetu wanapata matokeo mazuri zaidi kuliko miaka ya nyuma kwenye somo la Kiswahili, lakini safari bado ni ndefu. Kitu cha kutia shaka ni ongezeko la kukosekana kwa usawa kwenye matokeo ya kujifunza kutokana na maeneo wanayoishi watoto, kwani takwimu zinaonyesha mahali anapoishi mtoto panachangia kwa kiasi kikubwa uwezo wake wa kujifunza kuliko sababu nyingine ama kutokupata elimu ya mama yake au kutokuoata elimu ya awali.”
Aitha ripoti hiyo imetoa matokeo ya jumla katika kuoanisha uwezo, na jitihada za wanafunzi katika kusoma na kufanya hesabu, lakini pia imeonyesha wanafunzi wengi walio katika madarasa ya chini wapo nyuma ya matarajio ya mtaala pamoja na hali hiyo kutia matumaini.


Kwa upande mwingine ripoti imebainisha kushuka kwa kiwango cha uandikishaji wa watoto wa vijijini hasa katika miongoni mwa rika zote wakati kwenye maeneo ya mijini umeendelea kuimarika.


Zaida Mgalla, Meneja uwezo Tanzania anasema “Tunaipongeza serikali kwa jitihada zake za kuhakikisha watoto wanapiga hatua katika somo la Kiswahili pamoja na kuhakikisha watoto wengi wanapata vitabu, lakini hatupaswi kuridhika, kwani changamoto inayotukabili sote ni kuhakikisha tunapiga  hatua katika kuelekea ubora uliokusudiwa katika sekta ya Elimu, na kwa kujikita zaidi katika kuboresha matokeo ya kujifunza katika shule zetu”

Post a Comment

 
Top