Akizungumza na vyombo vya habari akiwa na waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, Roma mkatoliki
ameelezea jinsi walivyotekwa siku ya Jumatano na kufungwa pingu, kitambaa usoni
na baadaye kusafirishwa hadi eneo wasilolijua.
![]() |
Akizungumza kwa hisia na uchungu Roma alisema kuwa walipofikishwa walipopelekwa na kupata mateso mengi kwa kupigwa hadi siku ya Ijumaa usiku.
“Tukatolewa
tulimokuwepo siku ya ijumaa jioni na kufungwa uso, na mikono na miguu.
Tukapelekwa sehemu tukatupwa kwenye dimbwi la maji karibu na baharini Roma
anasema kuwa alipata fahamu na kuweza kuwafungua wenzake na kutembea mwendo
mrefu ambapo walifika katika maeneo ya Ununio” alisema
Roma Mkatoliki
Hata hivyo msanii huyo
alishindwa kuelezea baadhi ya maswali aliyoulizwa kuhusu kile walichokuwa
wanaulizwa na watekaji huku akisema kwamba tayari wamewasilisha malalamiko yao
polisi kwa uchunguzi, huku maofisa wa serikali walioandaa mazungumzo hayo na
wanahabari wakimzuia msanii huyo kusema lolote .
Katika mkutano huo Roma na wenzake walionyesha baadhi
ya majeraha waliyopata chini ya watu waliowateka na kusisitiza kwamba kile walichokipitia
sio suala la mzaha, wameitaka serikali kuwahakikishia usalama wao wakidai
kwamba licha ya kuwepo katika eneo lililozungukwa na watu maarufu ikiwemo
serikalini watekaji wao walifanikiwa kutekeleza tendo hilo bila wasiwasi.
Post a Comment