Kundi la raia kadhaa wa nchi ya Nigeria waliokuwa wakisafiri kwenye ndege ya shirika la KLM wakitokea Amsterdam schiphol airport nchini Uholanzi, walizuia ndege waliyokuwa wakisafilia ili raia mwenzao wa Nigeria aliyefungwa minyorororo atelemshwe.
Hali ya mabishano kutaka raia huyo atelemshwe hama afunguliwe ilikuwa kama matakwa kwa Wanigeria hao kuelekea kwa maofisa wa polisi ambapo yalizuka majibizano mara baada ya kumuona raia huyo wa Nigeria akiwa amefungwa pingu na minyororo kama mtumwa au mnyama.
Kundi hilo la Wanigeria baada ya kuwashinikiza kundi la maofisa wa usalama wapatao watano ambao kazi yao ilikuwa ni kumuondoa raia huyo hama sivyo ndege hiyo iendelee kubaki juu ya ardhi pasip
![]() |
PHOTO: Jamaa aliyekuwa kafungwa pingu ndani ya ndege ya KLM. |
Raia huyo inasemekana alikuwa akirudishwa nchini Nigeria kutokana na kutokuwa na nyaraka muhimu za kuishi au kufanya kazi nchini Uholanzi.
Hata hivyo baada ya mzozo kuonekana kukera abilia na watu wengine, hatimaye raia yule aliyekuwa amefumgwa minyororo aliteremshwa kutoka kwenye ndege ile na askari huku akiwa chini ya ulinzi.
Baadaye ndege iliendelea na safari.
Source: THE REPUBLICAN NEWS
Post a Comment