0
Na Mary Mwakibete –Mbeya.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla amepokea msaada wa mifuko ipatayo 400 ya saruji ikiwa ni hatua moja kutokana na ombi lake kwa Benki ya Akiba Commercial Ltd nchini tawi la Mbeya kusaidia ujenzi wa Hospitali ya rufaa kwa upande wa njia za wagonjwa zenye umbali wa mita 175.

PHOTO: Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla Akiongea wakati
katika hafla fupi ya kupokea msaada wa mifuko ya saruji jijini Mbeya,
kulia kwake ni Afisa masoko na uendeshaji wa Akiba Dora Saria.

PHOTO: Afisa masoko na Uendeshaji Dora Saria (wa kwanza kushoto) akongwa jambo wakati wa kukabidhi msaada wa saruji kwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla mwenye miwani.

PHOTO: Mmoja wa wafanyakazi wa benki Akiba akipokea mfuko wa saruji kutoka kwenye roli ili kuukabidhi kwa RC Makalla.




>>>>>>>>
Katika hafla fupi ya makabidhiano hayo, RC Makalla amewapongeza na kuushukuru uongozi wa Benki hiyo kwa jinsi walivyojitoa na kushugulikia maombi kwa haraka na kusaidia kuendeleza ujenzi uliokuwa umesimama kutokana kukosekana kwa fedha shilingi 55 milioni, hivyo msaada huo utakuwa na tija kwa mkoa wa Mbeya na ukanda mzima wa nyanda za juu kusini na nchi kwa ujumla.

Aitha Mkuu huyo wa Mkoa kupitia kwa marafiki wa hospitali ya mkoa wale wanaoishi nje ya mkoa huo wamekamilisha ujenzi wa mita 155 kupitia harambee iliyofanikisha ujenzi huo, ambapo katika ujenzi huo fedha zilizotumika ni shilingi 160 milioni za Tanzania.

“Kukamilika kwa ujenzi huu kutaondoa tatizo la wagonjwa kupelekwa au kwenda wodini kupita kwenye mazingira yasiendana na hali ya mgonjwa, pia wakati wa mvua na jua tatizo linakuwa kubwa” alisema RC Makalla.

Kwa upande mwingine afisa masoko na uendeshaji wa Benki ya Akiba Dora Saria amesema kutokana na wananchi kupata shida hasa wagonjwa kwenda wodini au kupeleka maiti kwenye chumba cha kuhifadhia marehemu kutokuwepo na njia rafiki, wao kama benki inayotoa huduma kwa wananchi waliguswa na kutokana na ombi la Mkuu wa Mkoa ambapo wamechangia shs 5milioni ambayo ni sawa na mifuko ya saruji 400.


Pia benki imevutiwa na jitihada za mkuu wa mkoa katika kuliweka jiji la Mbeya katika mazingira safi hivyo watatoa vifaa vya usafi na kushiriki kufanya usafi mwishoni mwa mwezi huu.


Post a Comment

 
Top