KONDOA
–DODOMA.
Mafunzo
ya walimu juu ya mtaala mpya ulioboreshwa kwa walimu wanaofundisha darasa la
tatu hadi la nne katika shule za msingi nchini yanayoendelea katika vyuo kadhaa
vya ualimu nchini yanaendelea katika chuo cha Ualimu Bustani kilichopo wilayani
kondoa ikiwa ni awamu ya tatu na mwisho kwa mafunzo hayo yanayotarajiwa
kukamilika mwanzoni mwa mwezi ujao kwa walimu kwa mkoa wa Dodoma.
PHOTO: Mkuu wa wilaya ya kondoa (katikati)
akiambatana na mkuu wa chuo cha Ualimu Bustani (kulia kwake) na (kushoto) Mratibu
wa Mafunzo Lucas Mzelela wakiongozana kuelekea ukumbini kufungua mafunzo.
|
PHOTO: Mratibu wa mafunzo ya KKK kituo cha Chuo cha Ualimu Bustani Kondoa akimkaribisha mkuu wa Wilaya kondoa kwa ajili ya ufunguzi wa mafunzo.
|
PHOTO: Mkufunzi wa mafunzo kutoka chuo cha
Uongozi ADEM Bagamoyo Pwani Mwalimu Esta Jonas akitoa taarifa ya mafunzo wakati
wa ufunguzi wa mafunzo kwa walimu kwa mkoa wa Dodoma.
|
PHOTO: Baadhi ya walimu wakifuatilia hotuba
kutoka kwa Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kondoa alipokuwa akifungua
mafunzo hayo.
|
PHOTO: Picha ya pamoja mkuu wa wilaya ya
kondoa (wa tatu kushoto) akiwa na viongozi wa ADEM na walimu wanaohudhulia
mafunzo, mara baada ya ufunguzi wa mafunzo.
|
Akitoa
taarifa za mafunzo hayo Mkufunzi wa mafunzo kutoka chuo cha mafunzo ya uongozi
kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani Esta Jonas amesema mafunzo hayo yamejikita
katika kuwajengea umahiri walimu wanaofundisha masomo ya Lugha na Hesabu walimu
wanaofundisha darasa la tatu na nne juu ya stadi Kuandika, Kusoma na Kuhesabu
(KKK) kwa njia ya uchopekaji ikishirikisha masomo mengine.
Katika
mafunzo hayo yalishirikisha waalimu kutoka wilaya ya Mpwapwa, Kongwa, Kondoa
mji, washiriki wote waliomaliza mafunzo na wale waliopo sasa wamekuwa wakipewa mtihani
kabla na baada ya mafunzo ili kuweza kuwapima uwezo wa umahiri.
“washiriki watapitishwa kujenga umahiri
katika maeneo kadhaa ikiwemo kupitia mtaala ulioboreshwa wa darasa la tatu na
nne, kupitia miongozo ya kufundishia, maandalizi ya ufundishaji, mbinu za
ufundishaji na kuchambu ili kutumia mbinu stahiki za ufundishaji
zinazoshirikisha wanafunzi katika ufundishaji na kujifunza” alisema Esta Jonas.
Wakati
huo huo mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo mkuu wa wilaya ya Kondoa Sezaria
Makota ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi amesema kwenye mkoa wa Dodoma washiriki
wote waliotakiwa kuhudhulia na kushiriki mafunzo hayo wamehudhulia kwa asilimia
100.
Aitha
ametoa wito wa walimu wanaoshiriki mafunzo hayo kutambua kuwa nafasi iliyopo ni
wao mara baada ya mafunzo hayo kwenda kuonyesha umahiri wa mafunzo waliyopata
na hatimaye Watanzania waone mwanga kwa wanafunzi wa darasa la tatu na nne.
“hili ni tukio
la kihistoria ikizingatiwa kuwa muda mrefu walimu wamekaa muda mrefu bila mafunzo hivyo hii inaleta picha
katika muelekeo wa elimu Tanzania kuwa na muelekeo mpya” alisema DC Sezaria Makota.
Vile
vile amewataka washiriki kutambua kuwa uwepo wa mafunzo yoyote kwa mfanyakazi
ni kulenga kuimarisha ujuzi na utendaji wa kazi kutoka kile unachojifunza na
kuwa mahiri zaidi, aliongeza kuwa “ndiyo maana serikali na wadau wa maendeleo wameamua
kuwekeza zaidi katika mafunzo kama haya, hivyo tunataka tuone mabadiriko katika
sekta ya elimu ‘mabadiriko chanya’ ili kuendelea kuoata mafunzo mengine, kama hakutakuwa
na mabadiriko miongoni mwenu baada ya mafunzo haya basi itakuwa ni upotevu wa
rasilimali fedha na muda”.
Mafunzo hayo yaliondeshwa
katika mikoa 7 hapa nchini yamekuwa na muitikio mkubwa na mzuri kwa walimu
ambao watakuwa na jukumu la kipekee katika kuufanya mtaala huo mpya kushika
kasi na kuwafanya wanafunzi kuwa na weledi wa kusoma, kuandika na kuhesabu huku
ushirikishi wa masomo mengine ukiingizwa wakati wa masomo (Kuchopeka) lengo ni
kumfabnya mwanafunzi aweze kuelewa na kusoma kwa hatua stahiki.
Post a Comment