"DUNIA
ITIMIZE WAJIBU WAKE KWA WANAWAKE NA WASICHANA 50-50 IFIKAPO MWAKA 2030"
PICHA 5: Matembezi ya kinamama wa jumuhiya ya Afrika mashariki wanaoishi na kufanya kazi jiji Arusha katika picha tofauti kwenye maadhimisho ya siku hii duniani.
Picha na Godfrey Thomas AR
HABARI KWA UNDANI:
Dunia
itimize wajibu wake kwa wanawake na wasichana 50-50 ifikapo mwaka 2030
Dunia inabadilika huku mabadiliko haya yakiwa na athari
kubwa kwa wanawake, lakini katika upande mwingine, maendeleo ya teknolojia na
utandawazi yanatoa nafasi kwa wale ambao hawana uwezo wa kutumia, hata hivyo
kunaendelea kushuhudiwa ongezeko kubwa la sekta za ajira zisizo rasmi, utofauti
wa kipato na hali tete ya kibinadamu.
Kwa hali hii ya kurudi nyuma, ni asilimia 50 pekee ya
wanawake wenye umri wa kufanya kazi ndio wanawakilishwa kidunia, ukilinganisha
na asilimia 76 ya wanaume ambao wanafanya kazi na kulipwa mshahara. Lakini cha
kushangaza zaidi wanawake wengi wameajiliwa kwenye sekta zisizo rasmi za
kiuchumi, wamekuwa ni watu wa kufanya kazi za nyumbani peke yake na kufanya
kazi zenye ujira mdogo na zisizo na usalama kwao.
Kutokana na hilo wanaharakati wa masuala ya wanawake wanasema
kuwa, kufikia malengo ya usawa wa kijinsia dunia, ni kazi ya pamoja ya watu
wote kwa maendeleo endelevu. Ndio maana umoja wa Mataifa kupitia maadhimisho ya
mwaka huu, unatoa wito kwa dunia kufanya kila namna kufikia usawa wa kijinsia
kuelekea dunia ya asilimia 50 kwa 50 ifikapo mwaka 2030 na kwa kuhakikisha kuwa
dunia ya kazi ni kwa wanawake wote pia.
Katika mkutano ujao wa taasisi ya wanawake wa umoja wa
Mataifa utakaoanza Machi 13 hadi 24 jijini New York, utaelezea uwezeshaji wa
wanawake kiuchumi katika kubadili mtazamo wa ajira ya dunia.
Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, anasema
kuwa haki za wanawake ni haki za binadamu, lakini akaongeza kuwa nyakati hizi
za mizozo dunia imekuwa haitabiriki na imeharibika, anasema haki za wanawake na
wasichana zimepunguzwa, zimewekewa ukomo na kubadilishwa.
Guterres anasema kuwawezesha wanawake na wasichana ndio njia
pekee ya kuwalinda na kulinda haki zao na kuhakikisha wanatimiza ndoto zao.
Wataalamu wanasema kupunguza ombwe la usawa wa kijinsia
kwenye ajira kutaongeza dola za Marekani trilioni 12 kwenye pato ghafi la dunia
kufikia mwaka 2025, na wanasema kwa kuongeza wigo wa wanawake kufanya kazi,
kutawafanya wawe wawakilishi wazuri, wabunifu na kuendeleza maamuzi yao kwa
jamii.
Suala la usawa wa kijinsia ni kiini na mzizi wa ajenda ya
mwaka 2030 ya Maendeleo Endelevu na kwamba ajenda namba 5 ya Maendeleo Endelevu
inasema wazi kabisa kuhusu usawa wa kijinsia na uwezeshaji kwa wanawake na
wasichana wote na kwamba ni muhimu kufikia mafanikio haya katika ajenda zote 17
za Maendeleo Endelevu.
Deep story source rfi





Post a Comment