**Kile ambacho Marvin Anderson
alitaka kukifikia katika maisha yake ni kuwa mzima moto, lakini badala yake
akiwa na umri wapata miaka 18, akawa ametuhumiwa kwa ubakaji, utekaji na wizi.
![]() |
PHOTO: Criminal Justice Reform ALB...
|
Ripoti
mpya iliyotolewa na Masjala ya Kitaifa ya Watu waliofutiwa hatia (NRE) ya mradi
wa pamoja kati ya Chuo Kikuu cha California - Chuo Kikuu cha Michigan, Shule ya
Sheria na Chuo Kikuu cha Jimbo ambayo ni Shule ya Sheria, inaonyesha kuwa kuna
uwezekano mkubwa kwa watu weusi kutuhumiwa na kufungwa bila ya makosa kuliko
watu weupe na pia wanaweza kukaa jela muda mrefu kabla ya kujulikana hawana
hatia.
Wakati
watu weusi wanawakilisha asilimia 13 ya idadi ya wananchi wa nchini Marekani,
lakini wana idadi kubwa ya watu waliofutiwa hatia katika daftari la masijala la
Taifa hilo, “katika
baadhi ya matukio, unaona wazi aina fulani ya ubaguzi,” amesema
Samuel Gross, Profesa wa Sheria, Chuo Kikuu cha Michigan. Wakati huohuo pia ni
mhariri wa ngazi ya juu wa ripoti hii.
Watafiti hao wamejikita katika vitu vitatu, ikiwa ni
kwenye makosa ya jinai ambapo watu weusi wamekuwa na uwezekano mkubwa kuliko
watu weupe kutuhumiwa kwa makosa ambayo hawajafanya, kuuwa, kubaka na makosa ya
madawa ya kulevya. Wakati wakikiri kuwa sababu zinazopelekea kusingiziwa makosa
wasiyo yafanya zina tofautiana kwa kiwango kikubwa kati ya kosa moja hadi
jingine, pia wanasema wamekuta aina za ubaguzi wa rangi katika makundi yote
matatu yaliyohusishwa na tafiti hiyo.
Kwa mujibu watafiti hao, watu weusi wasio na makosa
wana uwezekano mara saba zaidi kutuhumiwa kwa mauaji kuliko watu weupe, kwa namna fulani asilimia za kesi za mauaji
kati ya watu weusi ziko juu zaidi kuliko miongoni mwa watu weupe, na hivyo watu
weusi wasiokuwa na makosa wanauwezekano mkubwa wa kudhaniwa wametenda makosa na
kufungwa kwa mauaji.
Zaidi ya hilo, kesi za mauaji ambako mtuhumiwa mweusi
amehukumiwa kwa makosa ziko takriban asilimia 22 na inawezekana zikahusisha
uvunjifu wa sheria kwa upande wa polisi kuliko wale watu weupe waliotuhumiwa. Watu
weupe sio mara nyingi wanaweza kutambua nyuso za watu weusi nadharia ya upendeleo wa rangi yako katika mchanganyiko wa
kutambua rangi mchanganyiko.
Inapokuja katika makosa ya jinai ya dawa za kulevya,
watu weusi wanauwezekano mara 12 zaidi kufungwa kuliko watu weupe katika makosa
hayo, wakati makundi ya watu weusi na weupe wanaviwango sawa katika utumiaji wa
dawa hizo haramu, watu weusi wanauwezekano mkubwa kukamatwa na kufungwa kwa
makosa haya kuliko watu weupe, watafiti wamegundua hilo.
![]() |
| P PROFILE: Marvin Anderso katika picha tofauti kabla ya kifungo. |
Marvin Anderson ni mmoja kati ya mamia ya watu weusi
ambao wamehukumiwa na baadae kuachiliwa huru kwa makosa waliokuwa hawajafanya,
kile ambacho alitaka kukifikia katika maisha
yake ni kuwa zima moto/fire rescue, lakini badala yake akiwa na umri wapata miaka
18 akawa ametuhumiwa kwa ubakaji, utekaji na wizi.
Wakati jaji katika jimbo la Virginia alipotoa hukumu
atumikie kifungo cha miaka 210 anasema “Mwili wangu wote ulikufa ganzi” Anderson
alikiambia kituo cha Televisheni cha CNN.“Nilijua nitafungwa kwa kosa niliokuwa sijalifanya.
Ilinichukua
miaka 15 nikiwa jela na miaka mitano ya kuachiwa huru kwa masharti kabla ya
kufutiwa hatia baada ya vipimo vya vinasaba (DNA) kuthibitisha hakuwa na hatia.“Nilikuwa
naamini mfumo wa sheria lakini ukaniangusha,” amesema.
****Ubaguzi usiowazi pia ni
sababu inayopelekea hilo, Gross amesema.



Post a Comment