0
ARUSHA.
Semina ya ufugaji wa kuku kwa wafugaji wadogo na wakubwa na yenye lengo la kuwafanya wafugaji kuweza kuwa na mifugo isiyo na magonjwa ikiwa ni pamoja na ufugaji wa kitaalam imefanyika jijini Arusha katika eneo la Tengeru kwenye Chuo cha Ualimu Patandi kwa lengo la kuwapa ujuzi endelevu kuweza kutoa mazao bora ya kuku.





PICHA:  Matukio mbalimbali za wafugaji kutoka Tengeru mkoani Arusha wakiwa katika mafunzo jinsi ya kufuga kuku kwa kutumia mbinu za kisasa ikiwa ni pamoja na kutoa mazao bora ya kuku wasiyo na kemikali kwenye mifupa ambazo zinaweza kuwa na madhara kwa walaji hasa wanaopenda kutafuna mifupa.

PICHA:  Hamis Ally mkufunzi kutoka kampuni ya Ultravetis akielemisha wafugaji wa kuku (hawapo pichani) 

PICHA:  Wafugaji wakiwa makini kusikiliza na kuandika mambo muhimu katika mafuzo hayo. 

PICHA:  Mkufunzi wa mafunzo Hamisi Alyy kushoto, akitoa elimu kwa wafugaji (hawapo pichani) kulia ni mwakilishi wa kampuni ya Ultravetis.  

PICHA:  Wafugaji wa kuku waliohudhulia mafunzo hayo wakifuatilia maelekezo namna ya kupata mazao bora ya kuku. 

Moja ya dawa ambayo iliwagusa wafugaji ni Sd3, hii imeelezewa na Hamis Ally mtoa mafunzo kuwa haina madhara endapo kuku atakunywa ndani ya wiki moja kabla ya kupelekwa sokoni kwa kuuzwa.

Madhara yanayosema hapa ni yale ambayo mlaji huwa anashauliwa kutotafuna mifupa hasa ya kuku wa kisasa (kuku mzungu) kutokana na kukuzwa kwa kipindi kifupi cha wiki tatu mpaka nne hivyo kuonenkana kuwa kemikali nyingi zilizotumika kumkuza kwa spidi hiyo.

"Matumizi ya dawa hiyo huondoa sumu zote ndani ya kuku huyo hasa ile ndani ya mifupa ambayo watu wengi wamekuwa na hofu ya kutafuna" anasema Hamis.

Post a Comment

 
Top