0
PROFILE CARTOON: Sudani kusini alipokuwa anaomba kujinga na EAC.
Bunge la afrika mashariki limeweka wazi, suala la kuzorota kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika uwasilishaji na utoaji wa michango ambapo kutokana na hilo wameonya kuwa ikiwa hatua stahiki hazitachukuliwa haraka jumuiya hiyo itaelekea pabaya.

Baadhi ya mambo yanayochangia ni kutotekelezwa kwa miradi mbalimbali ya maendeleo, kutolipwa mishahara wafanyakazi wa jumuhiya hiyo kwa muda sasa, hizo ni baadhi ya changamoto zilizopo na zimeanza kujitokeza kutokana na nchi hizo kutochangia kwa wakati.

PHOTO: Bendera za nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki

Wabunge hao wamesema ingawa kumebaki miezi kadhaa ili mwaka wa fedha uishe, mchango uliotolewa haufikii hata nusu ya bajeti inayotakikana, hilo ndio limewafanya wabunge hao kuomba serikali za nchi wanachama kutoa maelezo na kutekeleza swala la utoaji wa michango kwani changamoto zinazidi kuongezeka.

Aidha licha ya mengi yaliyozungumzwa katika mkutano huo wabunge hao wamewaagiza mawaziri wa jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili haraka pamoja na viongozi wakuu wa nchi hizo ili kutatua jambo hilo.

Kwa upande wao mawaziri ambao pia wameudhuria vikao vya bunge wametangaza kwamba suala hilo linaenda kupewa uzito na muda si mrefu litajadiliwa na viongozi wa nchi. Wabunge hao wamesema serikali zinapaswa kujihadhari ili Jumuiya isije kuvunjika tena.




Source: rfi

Post a Comment

 
Top