![]() |
PHOTO:
Mwanasheria Laurence Masha ambaye amejitoa
kugombea nafasi ya Urais wa TLS na kumuunga
mkono mgombea mwenzake Tundu Lissu.
|
ARUSHA.
Hatimaye wakati wa
kujinadi na maswali ulifika kwa wagombea kuweka bayana maslahi yao kwa chama
hicho cha watetezi wa raia katika vyombo vya kudai haki, ambapo wagombea
walikuwa sita mmoja kati yao Laurence Masha yeye aliamua kujitoa na kumuunga
mkono Lissu kwa maslahi chama na wanachama wengine akidai kwa sasa chama
kinataka mtu mwenye nguvu na uwezo wa kukisaidia katika kusimamia haki.
Aitha wakati wote wa
kujinadi kwa mgombea mmoja mmoja, aliyeonekana kukonga mioyo ya wanasheria hao
kila alipokuwa akiongea alipigiwa makofi lakini hali ilikuwa ya hamasa hasa
pale aliposimama Tundu Lissu.
TODAYS NEWS tunakuwekea
video ambayo Lissu aliweza kujieleza, kujinadi na kujibu maswali kadhaa hapo jana jijini Arusha ilikuwa muda mfupi tu alipofika kutokea Dar Es Salaam, alipokuwa ameshikiliwa na jeshi la polisi kisha kupewa dhamana.

Post a Comment