0
Mambo mengi yamejitokeza hivi sasa kuhusu mtu mwenye umri wa miaka 52 ambae aliwaua watu wanne Jumatano na kuwajeruhi watu zaidi ya 12 wengine katika Daraja la Westminster na ndani ya Jengo la Bunge la Uingereza.


PHOTO: Khalid Mosood mtu aliyefanya mashambulio sehemu mbalimbali
nchini Uingereza na kuua watu kadhaa na kujeruhi wengi.
Chakula cha mwisho cha usiku alichokula kabla ya kushambulia ilikuwa ni kababu, aliokula katika mgahawa wa bei nafuu katika upande wa kusini wa pwani ya Brighton, kilomita 87 kutoka Uingereza.

Wafanyakazi wa hotelini alikokuwa amelala wamesema hapakuwa na kitu cha kumfanya mtu afikirie kwamba alikuwa katika jioni ambayo ataongeza jina lake katika orodha ya washambuliaji ambao wameuawa wakati wakifanya vitendo vya mauaji huko Ulaya.

Alikuwa mcheshi na mwenye furaha, na aliwaambia wafanyakazi kwamba anawatembelea marafiki Brighton, hoteli iliyoko pembezoni mwa bahari ambako watu wengi huzuru kwa masaa kadhaa na kurejea nyumbani na hivi karibuni eneo hilo lilikuwa linahusishwa na mashoga.

Meneja wa hoteli amewaambia waandishi gaidi huyo alikuwa “akicheka na akifanya mzaha akiwasimulia wapi aliishi” masaa kadhaa kabla hajafanya shambulizi.Lakini tabia yake ya uvunjifu wa amani pia inafahamika kuanzia vitendo vya ugomvi mpaka kumkata mtu usoni katika ugomvi wa kwenye baa.


PHOTO: Hoteli ya Preston Park Hotel huko Brighton ambako Khalid
Masood alikuwa amelala usiku kabla ya kufanya shambulizi.


MAISHA YA HUYU JAMAA.
Idhaa za televisheni za Uingereza Ijumaa zilionyesha picha za Khalid Masood alipokuwa shuleni, wakati huo akijulikana kama Adrian Russel Ajao jina la familia linalotokana na baba yake wa kambo.

UPDATE:
Mtu huyu alizaliwa siku ya Chrismas, 1964. Kama mtoto wa shule katika eneo lenye uchachamavu na kuvutia linalokaliwa na watu weupe zaidi alikuwa mpenzi wa soka, akicheza rugby, na akaingia katika kujenga misuli na pia aliwahi kujaribu madawa.

Rafiki wa utotoni wa mtu huyu ametoa fununu inawezekana akawa alikuwa mlengwa wa aina fulani wa ubaguzi shuleni.

“Alikuwa mwigizaji mkubwa,huku akipenda marafiki na kucheka,” Kenton Till ameliambia gazeti la Uingereza Daily Mail, lakini pia inawezekana akawa ndio mtoto wa kiafrika pekee katika shule hiyo, kwani alikuwa amepitia katika aina kidogo ya ubaguzi,” ameongeza kusema, lakini, “sio sana kwa sababu alijaribu kuwa maarufu.”

PHOTO: Khalid Masood katikati na kwenye duara akiwa katika shule ambayo haikuwahi kuwa na mtu mweusi lakini yeye aliweza kupata nafasi akiwa ni pekee.
Till aliendelea kusema kuwa: “Tulikuwa tukishirikiana pamoja mpaka tulipomaliza shule lakini aliwahi kuja kwenye sherehe nyumbani kwangu pamoja na baadhi ya marafiki baada ya kuvuta bangi na mama yangu aliwafukuza wote. Baada ya hapo tukapoteza kwa namna fulani mawasiliano.”


Katika siku za hivi karibuni baada ya kumaliza shule, alikuwa akifanya kazi katika shamba la familia, akiuza bidhaa za kusafishia na akawa anaishi na mwanamke ambae alikuwa mdogo kwake kwa miaka minne. Lakini baadae kwa sababu ambazo hazikuweza kufahamika kila kitu kikawa kimevurugika.


Polisi mara kwa mara walikuwa wanaitwa nyumbani wake, nyumba aliyokuwa anaishi na yule aliyekuwa wakati huo mke wake Jane Harvey, ambaye alimzalia watoto wawili kati ya watoto watatu wa Khalid Masood.

Marafiki waliliambia gazeti la Sun Newspaper kuwa Khalid Masood alikuwa akigombana kila alipokuwa amekunywa, lakini familia hiyo ikatengana mnamo mwaka 2000 baada ya Masood kumkata usoni mmiliki wa baa hivyo kupelekea kesi ambayo ilimfanya Masood afungwe kwa miaka miwili.


Muuaji huyu alilaumu ubaguzi kwa kupigana kwake, akiiambia mahakama alimkata mmiliki wa mgahawa huo usoni kwa sababu watu wa eneo alilokuwa anaishi katika kijiji cha East Sussex “walimuonyesha chuki” wakati huo alipokuwa anaishi huko.



**NEW LAST
Nimekuwekea habari//story ya muendelezo wa hapa katika page nyingine ili iwe rahisi kujua UPDATE yake.



Source BBC.


Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top