Mfumo wa Chama, una sura ya serikali na utawala na kuwa na ngazi nyingi ya vikao vya uamuzi. Hali hii inafanya gharama ya kukiendesha Chama kuwa kubwa, vikao haviitishwi na maamuzi ya chama hayawafikii walengwa. Hivyo basi yafuatayo yanazingatiwa,
Na Humphreys
Polepole. -II
Kupunguza wingi wa vikao vya nadharia na badala yake
kuwa na vikao vichache vinavyofanyika, vyenye maamuzi yenye tija na kujenga
uhai wa chama.
Kupunguza idadi ya wajumbe au
wawakilishi ili wawe wachache lakini wenye umakini na uwezo wa kusimamia sera,
itikadi, maamuzi ya chama pamoja na kuondoka urasimu na kupunguza gharama za
uendeshaji pasina kuathiri ubora wa uwakilishi. Muundo wa Wilaya za Chama
uendane na uundo wa sasa wa wilaya za Serikali
Uztio mkubwa umewekwa katika
kuimarisha chama katika ngazi ya shina, eneo ambalo ndilo waliko wapiga kura.
Kwa kufanya hivyo, chama kitakuwa karibu na watu na watakiona kuwa ni chama
chao. Uendeshaji wa shughuli zote za
jumuia za chama na mali zake uwe chini ya usimamizi wa Chama cha Mapinduzi na
Baraza la Wadhamini la Chama cha Mapinduzi.
Viongozi wachache wamekuwa na tabia ya kujilimbikizia
nafasi nyingi za Uongozi, utendaji na uwakilishi katika Chama na Serikali. Hali
hii hushusha ufanisi na kupunguza tija. Nafasi nyingi kwa mtu mmoja ni
kushindwa kuleta ufanisi katika vikao husika.
Hapa imezingatiwa kuwa;
ukiacha wale wanaolazimishwa kikatiba kuwa na nafasi zaidi ya moja kwa mujibu
wa mamlaka yao, kuanzia sasa nafasi za Uongozi katika chama zitakuwa si zaidi
ya moja.
Mfumo wa kura za maoni hukusudia kuimarisha demokrasia
ndani ya chama na kuashiria nafasi ya mgombea anayeonekana kukubalika zaidi, hata hivyo, eneo hili limekuwa na matokeo mabaya ya kukithiri kwa rushwa na
kupata viongozi wasio na imani ya kweli ya chama wanaosaka maslahi,
wafanyabiashara wenye malengo binafsi na mamluki.
Mapendekezo ya kuimarisha
udhibiti wa kura za maoni; -
Katiba ya CCM ya Mwaka 1977
Toleo la 2012 Ibara ya 61A(1-3) inaelekeza kura za maoni za ubunge na
uwakilishi zitapigwa kwenye mikutano mikuu ya jimbo na si kwa wanachama wote
matawini kama ilivyofanyika mwaka 2015.
Imependekezwa ili kudhibiti
taratibu za kura za maoni jimboni, kuepusha migawanyiko, kuziba mianya ya
rushwa na kuepusha wapiga kura mamluki, inapendekezwa kufanya mabadiliko ya upigaji
kura za maoni za ubunge na uwakilishi pamoja na kufuata utaratibu ufuatao wa
kuwajadili wanaogombea;
Wagombea ubunge/uwakilishi
watachukua fomu na kurudisha kwa Katibu wa CCM wa Wilaya inayohusika, fomu zote
za wagombea ubunge/uwakilishi zitajadiliwa na kutolewa mapendekezo katika ngazi
ya wilaya, mkoa na Taifa kabla ya kupigiwa kura za maoni.
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu
ya Taifa itateua majina yasiyozidi matatu ambayo yatawasilishwa mbele ya
Mkutano mkuu wa Jimbo kwa ajili ya kupigiwa kura za maoni. Mkutano mkuu wa
Jimbo utapiga kura za maoni kumpendekeza mwanachama mmoja awe mgombea wa ubunge/uwakilishi
katika jimbo hilo.
Mara ya baada ya kura za
maoni, mapendekezo ya uteuzi yataanzia kwenye Kamati ya Siasa Jimbo (kwa
Zanzibar), Kamati ya Siasa ya Wilaya (Tanzania Bara), Mkoa, Kamati Maalum (Kwa
Zanzibar), Kamati Kuu na hatimaye Halmashauri Kuu ya Taifa itafanya uteuzi wa
mwisho.
Utaratibu huu hautawapa fursa
wagombea kutengeneza makundi na kutoa rushwa kwasababu hakuna anayejua kama
atakuwepo kwenye orodha ya wagombea. Wale wana CCM wenye tabia ya kujiandaa na
vyama zaidi ya kimoja, kwa utaratibu huu hawataweza kujiandaa mapema kuhamia
vyama vingine. Utaratibu huu pia utasaidia kuondoa urasimu na migawanyiko
isiyokuwa na sababu.
Aidha, utaratibu huu
utahakikisha anapatikana mgombea mwenye msimamo thabiti wa Chama na ni
utaratibu halisi kwa chama kuusimamia ipasavyo.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.