 |
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara
Evod Mmanda Herman akifungua mkutano wa kwa niabda ya mkuu wa mkoa wa Mtwara
ambaye hakuwepo mapema leo mjini mtwara. |
 |
Wakurugenzi wa wilaya za Mtwara, Tandaimba,
Nanyumbu, Masasi na kutoka Lindi wakifuatilia hotuba.
|
 |
Mganga mkuu wa mkoa wa Mtwara Dr.
Lunemo akizungumza mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa utambulisho wa uboreshaji
huduma ya Afya.
|
 |
PICHA JUU NA CHINI: Baadhi ya wataalamu wa Afya na wahudhuliaji
wa mkutano huo kutoka wilaya za mkoa wa Mtwara uliofanyika Naf Hotel Apartment
mjini Mtwara.
|
 |
Wakurugenzi, Madaktari, wakiwemo
wawakilishi wa taasisi binafsi zinazojihusisha na utoaji huduma kwa jamii
pamoja na viongozi wa serikali wakimsikiliza hotuba za mkutano huo.
|
MTWARA.
Mkutano wa siku moja wenye lengo la kuhamasisha uboreshaji wa afya ya jamii unaofadhiliwa na mfuko wa msaada
wa watu wa Marekani unafanyika mkoani Mtwara ambapo umefunguliwa na Mkuu wa
mkoa wa Mtwara ambaye aliwakilishwa na mkuu wa wilaya ya Mtwara Evod Mmanda
Herman ambaye ametanabaisha nafasi ya elimu hiyo kuwa imekuja kwa wakati
muafaka.
Akifungua mkutano wa utambulisho
wa mradi huo mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa mradu huo wa USAID boresha Afya
utajikita zaidi kwenye ufadhili za huduma za VVU na Ukimwi, Kifua Kikuu, uzazi
wa mpango, uhamasishaji wa rasilimali, kupambana katika kuweka sawa masuala ya
jinsia, ambapo kwenye upande huo wa jinsia mradi unalenga hasa kwa kinamama na
watoto pamoja na masuala ya lishe na maboresho kwenye huduma za Afya kwa
ujumla.
“mradi huu ni mkubwa nawenye fedha nyingi ambazo kila mkoa
unatarajia kupata zaidi ya shs 30bilioni ili kuweza kuendeleza mradi huu ambao
unachangamoto mtambuka ndio maana umelenga kwenye hayo maeneo ni kwa sababu
yana nafasi muhimu sana katika athali ya Ukimwi, kwa sababu mtu alieambukizwa
VVU ni lazima akingwe na magonjwa nyemelezi” amesema
DC Herman.
Hata hivyo wakati
uboreshaji huo ukihusisha maboresho ya utoaji wa huduma kwa mkoa wa Mtwara bado
kuna nyanja kadhaa ambazo zitapewa kipaumbele ni kupitia shirika hilo la USAID
pamoja Deloitte ni kufanya kazi pamoja na Halmashauri zote za mkoa wa Mtwara
ikiwemo ofisi ya Mganga mkuu wa Mkoa ili kuweza kuwafikia wananchi wengi waliopo
sehemu zinazoweza kufikiwa na mradi huo.
Jofrey Tarimo ni
Daktari na Meneja wa ufundi wa kanda wa shirika la USAID Boresha Afya
anasema mradi huo utajikita kuweza
kupambana na vvu ikiwa ni kuweza kuwasaida wananchi kujikinga na ugonjwa huo,
lakini pia mradi utasaidia katika nyanja ya uzazi wa mpango na kuhakikisha
wananchi watakao kuwa tayari kupewa huduma na elimu waweze kuipata kwa wakati,
sehemu na kupitia mtu sahihi.
Dkt, Geofrey Tarimo
amesema “wale
wote watakaokuwa tayari kupata huduma hizi tunataka wazifikie bila vikwazo,
lakini sula la Maleria tutashugulika nalo ukizingatia Mkoa wa Mtwara ni kati ya
mikoa yenye maambukizo ya hali ya juu kwa ugonjwa wa Malaria, ambapo mradi huu
wa miaka mitano ulioanza tarehe 01.10.2016 na unatarajia kufanya katika mikoa
ya Mtwara, Lindi, Morogoro, Ruvuma, Iringa na Njombe”
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.