0
Profile PHOTO: Mshare ukielekeza kwenye mabadiriko.
Uchafuzi wa hali ya hewa umeendelea kutajwa kuwa changamoto ambazo zimeendelea kuzikabili nchi nyingi barani la Afrika ambapo kwa mujibu wa shirika moja la umoja wa Mataifa linaloshugulikia mazingira, limezitaka nchi za Afrika kuwekeza katika miundombinu ili kuweza kuwaruhusu wananchi kutembea kwa miguu au kutumia aina ya usafiri wa baiskeli.

Matumizi ya kutumia miguu na baiskeli itakuwa mojawapo ya njia itakayoweza kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa unaotokana na matumizi ya usafiri wa magari, vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya petroli au dizeli vinatoa gesi joto ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuongezeka kwa joto dunianil.

PHOTO: Mabadiriko ya mazingira na Athali zinazoikabili dunia.
Katika bara la Afrika ujenzi wa miundo mbinu kama ya barabara mfano katika jiji la Dar Es Salaam na Arusha inaonyesha kuwepo na njia zitakazoweza kutumika kwa watu watakaotumia miguu au baskeli ambazo hazitumii mafuta yoyote yale hivyo haina mchango wowote katika uchafunzi wa mazingira, lakini matumizi ya baiskeli hama na kutembea kwa miguu hubolesha Afya za wananchi, sababu iankuwa ni sehemu ya mazoezi


Kuna nchi ambazo ni hatari zaidi unapotembea kwa miguu au kwa kutumia usafiri wa baiskeli, Malawi ni nchi ya kwanza kwa mtu kutumia usafiri huo huku ikifuatiwa na Kenya ya tatu ni Afrika Kusini ambapo katika utafiti uliofanywa hivi karibuni umeonyesha kutokuwepo kwa njia za watembea kwa miguu au waendesha baiskeli hivyo mazingira hayo yanaweka ugumu kwa raia wa nchi hizo kutokuwa salama wanapotembea au kutumia baiskeli.





Kwa msaada wa rfi

Post a Comment

 
Top