Warsha ya mafunzo namna
ya kushugulikia kesi na matatizo ya ukatili, unyanyasaji wa kijinsia kwa
wanawake na watoto, imefunguliwa jijini Arusha ikiwa ni mafunzo ya kipekee kwa
wakati huu ambapo ambapo matendo ya ukatili wa kijinsia yamekithiri kwa kiasi
kikubwa katika jamii hapa nchini.
ARUSHA.
![]() |
PHOTO: Mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian
Daqarro.
|
Akifungua
mafunzo hayo, kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo,
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Fabian Daqarro amesema wakati kuna sheria
mbalimbali za kitaifa na kimataifa zikiwepo nyingine ambazo zitasaidia kuongeza
uelewa na ufahamu wa jinsi ya kushugulikia kesi za ukatili wa kijinsia mafunzo
hayao yawe ni msaada wawapo mahakamani ili kuongeza ufahamu na kuweza kusaidia
kuboresha ufanisi wa kazi mahakamani na kwenye jamii.
“Mafunzo haya yanalenga kuangalia namna gani mahakimu na majaji
wanawake wanaweza kuongezewa ujunzi, mafunzo na namna ya kwenda kushugulikia
haya matatizo sugu katika jamii yetu, sababu hata hapa wilayani kwetu Arusha
haya matatizo yapo ya watoto kulawitiwa, kubakwa, kudhalilishwa, kupigwa,
kuonewa, mirathi na kunyang’anywa mali haya
ni matatizo ambayo kupitia mafunzo haya tutapata msaada kuweza kutatua hali hii” amesema Daqarro.
![]() |
PHOTO: Iman Aboud, Mwenyekiti
wa chama
cha majaji na wahakimu wanawake nchini.
|
Mafunzo hayo yameshirikisha viongozi mbalimbali kutoka sekta za kijamii, wasimamizi wa
sheria, polisi, mawakili wa serikali na wakujitegemea, vyombo vya usalama,
watoa haki majaji na mahakimu pia wakiwepo viongozi wa dini, lengo likiwa ni
kuwapa uwezo katika kushugulikia masuala ya kijinsia na ukatili.
Jaji na Mwenyekiti wa Chama
cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania Iman Aboud anasema huu ni muendelezo wa
jitihada zilizoanza toka mwaka 2000 ambapo chama kilianza huku jitihada ikiwa
ni kumfanya mwananchi kutambua haki zake hasa pale anapofanyiwa ukatili na namna gani atamtetea mtoto wake hama mirathi yake.
Jaji Aboud anasema “washiriki
katika warsha hii pia tumewajimuisha viongozi wa dini mbalimbali tukiamini
kabisa nao wanapokuwa katika nafasi zao kama watu wanaojenga jamii,
wakizungumza katika sehemu zao misikitini, makanisani watasaidia sana, na sisi
kama wanawake tunalichukua jambo ili kwa uzito mkubwa ukizingatia sisi ni wana
taaluma siyo wana harakati ndiyo maana tunajikita katika kutoa Elimu, na
tunatoa elimu tukizingatia ukomo ambao sisi kama majaji tunakuwa nao”.
Warsha hiyo ya
siku tatu inategemewa kuwa msaada kwa washiriki wa mafunzo kuwapa njia itakayoweza kuifanya jamii kuwa na uelewa wa
namna ya kujilinda na kujikinga dhidi ya unyanyasaji unaofanyika katika jamii,
hata hivyo mafanikio yanayotokana na mafunzo haya mpaka sasa yanaonekana ni
makubwa kutokana na maamuzi yanayofanywa sasa na vyombo vinavyotoa haki
kuonekana kutoka katika ngazi ya chini.



Post a Comment