![]() |
| PROFILE PHOTO: DR CONGO |
Maofisa wa Jeshi la polisi wapatao 40
wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameuawa kwa kukatwa mapanga na wanamgambo
wa kundi la Kamwina Nsapu katika jimbo la kati la Kasai ijumaa ya juzi.
Kwa mujibu wa rais wa bunge la Kasai Francois Kalamba,
wanamgambo hao waliushambulia msafara wa magari ya polisi uliokuwa njiani
kutoka mji wa Tshikapa kuelekea mji mkuu wa jimbo la Kasai wa Kananga
waliposhambuliwa wanamgambo hao.
Kalamba amesema walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa
wanamgambo waliwaachia huru maofisa sita kwa vile walikuwa wanazungumza lugha
ya Tshiluba inayotumika eneo hilo, pia wanamgambo hao ambao kawaida huwa na
mapanga, waliiba bunduki na silaha za polisi kisha na kukimbia pamoja na magari
yao.
Uasi katika eneo la kati ya nchi ya DRC ulianza mwezi
Agosti mwaka uliopita 2016 na umeenea katika majimbo kadhaa ya eneo hilo. Hata
hivyo siku ya (jana) Jumamosi wizara ya mambo ya ndani ya serikali ya nchi hiyo
imetangaza kwamba kuna wanamgambo 400 wamejisalimisha kwa wiki hii katika jimbo
hilo la Kasai.


Post a Comment