Katibu mkuu wa balaza la Sanaa
la Taifa BASATA Godfrey Mngereza ametoa taarifa za kuufungia wimbo wa msanii wa
nyimbo za bongo freva Nay wa Mitego aliyetoa wimbo mpya uliobeba jina la ‘WAPO’
kuwa hauna maadili.
DAR ES SALAAM.
Katika taarifa yake amesema
wimbo huo unavipengele vinavyochochea vurugu pia hauna maadili kwa jamii ya watanzania
lakini pia sheria inachukua mkondo wake, ameongeza kuwa kukamatwa kwa Nay
hakutokani na wao Basata tu, maana sheria inagusa sehemu nyingi kwani Basata ni
serikali na hata waliomkamata ni serikali pia.
Aitha amesema maamuzi
wanayochukua ni kuzuia wimbo amabo hauna maaadili hata radio.“anayekamatwa na
ngozi ndiye mwizi, kwani katika utangazaji kuna (ethics) kanuni zake , hivyo
nikisikia kituo kinaupiga basi atakayepatikana kuupiga nayeye atahusika katika sheria, kazi ambayo
inatukana watu, inachochea vurugu hata kama hujamtaja mtu jina moja kwa moja, inavunja
sheria na maadili nitashangaa kusikia kazi chafu inapigwa na mtu mzima mwenye
akili timamu tena anasikiliza, sasa kutokana na hilo unajenga kizazi cha namna
gani ?” alisema Godfrey Mngereza.
Hapa nchini sheria kwa kuanzia na sheria mama ambayo ni katiba ya nchi zipo na zinazuia mtu kutukana adharani au
vitu visivyo na maadili ya mtanzania, hivyo basi mkono wa sheria ni mrefu unaweza
kukuchukua pale wanapoona unafanya makosa ya kuvunja sheria za nchi.
Hata hivyo kutokana si mara ya kwanza kwa Nay kukamatwa kutokana na makosa tofauti yakiwemo ya kutoa nyombo zisizoendana na maadili ya kitanzania hali hii itapelekea kupewa adhabu ambayo BASATA watakaa na kushauliana na
wanasheria ili kuona hatua gani stahiki watamchukulia.

Post a Comment