0
PHOTO PROFILE: MP Godbless Lema.

ARUSHA.
Mahakama kuu ya kanda ya Arusha leo imemuachia huru mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema kwa dhamana ikiwa ni baada ya mwezi/wiki iliyopita jopo la majaji watatu wa mahakama ya rufaa walitoa kalipio kali siku ya Jana dhidi ya ofisi ya DPP baada ya mawakili wa upande wa Jamuhuri kuondoa rufaa yao mahakama hiyo ya rufaa ilitoa uamuzi kwamba kesi hiyo irudishwe mahakama kuu ili iweze kumpa dhamana Mbunge huyo.



Kufuatia hali hiyo ya kuzuia dhamana ya mbunge huyo pasipo jambo la msingi, leo Lema ametimiza mashariti yote ya dhamana ambapo hapo awali alitakiwa awe na wadhamani wawili na fedha kiasi cha shilingi 3milioni.

Itakumbukwa kuwa Lema alikamatwa toka mwaka jana mwezi wa 11. 2016 kutokana na kauli za uchochezi alizotoa dhidi ya Rais Magufuri katika maeneo mbalimbali akiwa katika mikutano ya hadhara, ambapo aliwekwa mahabusu kwenye gereza la kisongo lililoko pembezoni mwa jiji la Arusha.






Post a Comment

 
Top