0
**Chama cha wasindikaji wa vyakula nchini kimewataka wafanyabiashara wajasiliamali kuongeza ubora wa bidhaa zao ili kuweza kufikia masoko makubwa hasa ya nje ya nchi hatua itakayo ongeza nafasi wigo wa biashara na mapato kwa mtu mmoja mmoja na taifa kupata mapata kutokana na masoko yao.

Mwenyekiti wa shirikisho la wasindikaji wa chakula nchini Suzy Laizer akiongea na wafanyabiashara wajasiliamali jijini Arusha.

Aliyesimama ni Suzy Laizer (Mwenyekiti Taifa), Hulda Kombe (Mwenyekiti Tafopa Arusha), Restituta Mrosso (Katibu Tafopa Arusha) na Msafiri Mshigheni  (Afisa uwekezaji wa jiji -Arusha)

PICHA JUU NA CHINI: Baadhi ya wafanyabiashara wa bidhaa za kusindikwa wakimsikiliza mwenyekiti Suzy Laizer (hayupo pichani) juu ya masoko na kunyanyua ubora wa bidhaa.

Wajasiliamali/Wafanyabiashara wa jijini Arusha wakiwa na bidhaa wanazozalisha




ARUSHA.
Akiongea na wafanyabiashara hao jijini Arusha, mwenyekiti wa chama hicho Taifa Suzy Laizer amewataka wafanyabiashara hao kutumia fulsa zilizopo katika kukuza ubora wa bidhaa na kuondoka na mawazo ya kusubili msaada kutoka kwa viongozi wanaokwenda kuwatembelea katika maeneo yao ya uzalishaji.

“wakati umefika kila mjasiliamali lazima atambue nafasi aliyonayo kutokana na kwamba, kwa sasa serikali imetoa nafasi kila mkoa kuwa na vikundi vya wakina mama ili kuwawezesha kukua zaidi kupitia mazao na bidhaa wanazozalisha kufikia ngazi ya juu” alisema Suzy.

Serikali imetenga fungu la bajeti la asilimia 5 kwa kila halmashauli nchini kuelekezwa kwa kinamama walio katika vikundi kwa lengo la kuwawezesha kufikia malengo makubwa ya uzalishaji wa mazao na bidhaa wanazozalisha, hii ni fulsa moja wapo inayoendana na kaulimbiu ya serikali ya awamu ya tano ya kuelekea kwenye uchumi wa viwanda.

Chama hicho ambacho kilianzishwa mwaka 1997 kikiwa na kinamama tu ambapo mpaka sasa kinashirikisha kinababa, kikiwa na lengo la kuleta kwa pamoja sauti ya wasindikaji wa chakula wa kawaida kuweza kusikika na kukabiliana na vikwazo katika usindikaji wa vyakula vya viwandani.

Pamoja  na kuanzishwa kwa chama hicho, baadhi ya wafanyabiashara wakubwa na wenye asili ya asia walikuwa na tabia ya kukataa kupokea bidhaa za ndani zilizozalishwa na wazalendo huku wao wakiweka bidhaa zilizozalishwa na wao wenyewe au kutoka nje kwenye masoko makubwa (supermarket)

Wakati huohuo mwenyekiti Tafopa mkoa wa Arusha Hulda Kombe anayezalisha unga wa mahindi usiokobolewa (DONA) amewahimiza wafanyabiashara hao kujiunga katika chama hicho ili kuweza kutambulika na kupata nafasi za fulasa zinazojitokeza ndani ya chama hicho.

“wakati wazalishaji wa ndani wanazalisha bidhaa bora, hali hiyo ilipelekea kudumiza wazalishaji wa ndani zikiwemo bidhaa za ndani ya nchi” anasema Hulda.

Post a Comment

 
Top