Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya ISTEP yaendesha
warsha ya mafunzo katika nyanja ya mazingira, masoko pamoja na kuwezesha
wataalam walio katika sekta ya elimu kupitia wakufunzi kutoka vyuo vya ufundi
nchini kuangazia utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati mbadala ili
kuweza kupunguza uchafuzi wa mazingira.
Warsha hiyo inayofanyika kwa siku tatu jijini Arusha imewakutanisha
wadau na wakufunzi kutoka mikoa kadhaa nchini na wadau wengine kutoka Taasisi
ya vyuo Canada (CICan), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (MOEST) na
Serikali ya Canada kwa pamoja wanaendesha warsha hiyo ikiwa ni sehemu ya
kuendeleza mazingira na kukabiliana na Tabia nchi.
Hapa chini tunakuletea baadhi ya matukio katika picha ambayo
yamejiri wakati wa warsha hiyo inayofanyika katika Hotel ya VETA Njiro jijini Arusha.
ARUSHA.
![]() |
Dr, Alan Copeland (aliyesimama kashika kiuno) ni Mtaalam mwandamizi wa ufundi
kutoka I STEP Tanzania, akisimamia mada inayohusu mazingira endelevu na nafasi
ya zana kwa taasisi, idara na wizara.
|
![]() |
Akichangia mada ya faida, hasara zitokanazo na
matumizi ya Solar na Genereta, Dr. John Msumba (kulia) kutoka Taasisi ya
Teknolojia na Ufundi (DIT) kushoto ni Dr Alan Copeland wakiangaliana.
|
![]() |
Dr. John Msumba kutoka Taasisi ya Teknolojia na Ufundi
(DIT) akifafanua umuhimu wa kutumia nishati ya jua katika matumizi mbalimbali
ili kuepukana na garama zinazoweza kuepukika.
|
![]() |
Wakiteta jambo la furaha kulia ni Happiness Salema,
mama Mbwambo na Leah Lukindo wakati mapumziko mafupi.
|
Baada ya ufunguzi wa warsha iliyokusanya wataalam na
wakufunzi wa elimu kutoka vyuo kadhaa nchini vya VETA pamoja na biashara wakiwa
katika picha ya ukumbusho katika hotel ya VETA Njiro jijini Arusha.
|
PICHA NA: Todays Production
+255 757 800 307
ARUSHA.
Warsha hiyo inayofanyika kwa siku tatu jijini Arusha
imewakutanisha wadau na wakufunzi kutoka mikoa kadhaa nchini na wadau wengine
kutoka Taasisi ya vyuo Canada (CICan), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
(MOEST) na Serikali ya Canada kwa pamoja wanaendesha warsha hiyo ikiwa ni
sehemu ya kuendeleza mazingira na kukabiliana na Tabia nchi.
Wakati nchi ikiwa katika
mchakamchaka wa maendeleo kwenda kwenye uchumi wa viwanda ambapo pasipo utunzaji
wa mazingira ni vigumu kufikia hatua inayotakiwa, wakati moja ya ajenda
inayojadiliwa katika warsha hiyo ni utunzaji wa Mazingira, likiwepo suala la Maji
pamoja na Nishati.
Leah Mkimbo ni
mkurugenzi wa mafunzo VETA anasema “sisi
kama watoa mafunzo suala la mazingira tunalipa kipaumbele sana, na lipo katika
mitaala yetu ambapo kupitia ushirikiano na vyuo vya Canada, wanatujengea uwezo kutokana
nafasi yao kuwa wanafanya vizuri kwa upande huo, ukiona mwenzako anafanya
vizuri, usikae mwenyewe bali jifunze kutoka kwake”.
![]() |
| Leah Mkimbo Mkurugenzi wa mafunzo VETA |
Wakati maji yanayotoka
katika mfumo wa maji taka wa majumbani yanaweza kufanyiwa mpangilio mzuri na
kurejea katika matumizi mengine kama kwenye bustani hama hata katika matumizi
ya ndani, hivyo basi mifumo kama hiyo ndiyo inapaswa kuingizwa katika mitaala ili
wanafunzi wanaomaliza na kurudi mtaani waweze kuwafundisha wananchi namna ya
kutumia hii mifumo.
Nishati ni kitu muhimu
katika maendeleo yoyote hasa katika uchumi wa Viwanda, na garama ya nishati
inayotumika ni kubwa sana, wakati umeme unaotumika nchini unatokana na maji na
kuna baadhi ya wananchi hawapati huduma hiyo hivyo nishati mbadala inayotokana
na jua, upepo na takataka ambapo umeme wake unawezaz kutumika sehemu yoyote na
kwa garama nafuu baada ya kufunga vifaa vinavyohitajika.
![]() |
Afridon Mkomoi -VETA Shinyanga.
|
Hata hivyo changamoto ni
kubwa katika nchi zinazoendelea kutokana na uharibifu wa mazingira
unaosababisha mabadiriko ya tabia nchi, hali hii inaweza kuleta tija endapo
taasisi zinazotoa mafunzo ziwawezeshe wale wanaopewa mafunzo kwa kiasi kikubwa
ili waweze kutoa elimu kwa mifano itakayozaa matunda na baadaye mafunzo
watakayopewa wananchi wanaozunguka eneo husika waone kupitia kile mtoa mafunzo
ananchomaanisha.










Post a Comment