Mwezi Novemba mwaka uliopita, alizuiwa jijini Nairobi
nchini Kenya wakati anajiandaa kubadili ndege kwenda jijini Kigali, baada ya
serikali ya Rwanda kuitaka Kenya kutomruhusu kufika Kigali.
![]() |
PHOTO: Kiongozi wa Upinzani
anayeishi nchini Ufaransa Thomas Nahimana.
|
Reuters.
Hali ya sintofahamu imeripotiwa nchini Rwanda baada ya
kasisi wa zamani ambaye kwa sasa ni kiongozi wa upinzani nchini humo Thomas
Nahimana, kutangaza kuunda serikali sambamba na utawala uliopo madarakani wa
Rais Paul Kagame.
Thomas Nahimana amechukuwa uamuzi huo baada ya kupigwa
marufuku kuingia nchini humo kujiandikisha kama mgombea wa kiti cha urais
katika uchaguzi mkuu unaopangwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.
Kiongozi uyo wa upinzani ambaye kwa sasa yupo
uhamishoninchini Ufaransa anasema lengo la serikali yake ni kuiondoa madarakani
serikali ya Rais Paul Kagame, wakati Thomas Nahimana amekuwa akiushutumu
utawala wa Paul Kagame ya kwamba unavunja sheria na kukandamiza wananchi.
Mwanasiasa huyo ambaye anatumia pasi ya kusafiria ya
Ufaransa, tayari ametangaza nia ya kuwania urais nchini humo mwezi Agosti mwaka
huu, hata hivyo hivi karibu alitarajiwa kurejea nchini Rwanda akitokea jijini
Brussels nchini Ubelgiji, lakini hakuweza kufanya hivyo baada ya kudai kuwa serikali
ya Kigali inaendelea kumwekea vikwazo.
Yves Butera, msemaji wa Idara ya Uhamiaji nchini
Rwanda wakati huo alisema kuwa Padri huyo atakaribishwa nchini Rwanda kama raia
mwingine, hata hivyo kiongozi huyo wa upanzini Thomas Nahimana amesema kuwa
serikali yake itakua ikifanya kazi ikiwa uhamishoni.
Fist appeared from rfi

Post a Comment