Uamuzi
wa kwanza wa msingi ni Kama Mkuu wa Mkoa anayo mamla kisheria kuagiza watu
wakamatwe na kuhusika moja kwa moja katika kufanya uchunguzi katika masuala
yanayohusiana na dawa za kulevya? na jambo hilo limepangiwa tarehe ya
kusikilizwa wiki ya kwanza ya mwezi Machi.
![]() |
| PROFILE PHOTO: Freeman Mbowe |
DAR ES SALAAM.
Jambo la pili lilikuwa ni kutaka basi hadi
hapo suala la msingi litakaposikilizwa wazuie wasiweze kunikamata au kunisumbua
kwa njia yeyote kunipa haki zangu za Kikatiba haki zangu za kisheria kwa sababu
wanaohusika kutenda tendo hilo hawana mamlaka hayo kwa maana ya Mkuu wa Mkoa na
wasaidizi wake, kwa hilo mahakama imekubaliana na mimi na imetoa zuio kwa
Polisi kunisumbua kwa njia yeyote ile hadi hapo Mahakama itakapokuwa imeamua
kama wana haki ama hawana haki.
Tulifungua shauri hili tokea tarehe
10/2/2017 mpaka leo ni tarehe 21/02/2017 ni siku 11 zimepita katika kipindi
chote hiki Polisi wamekuwa wanazunguka sana tunamtaka Mbowe tunamtaka Mbowe,
Mahakama ina uwezo wa kujipangia kalenda yake yenyewe ambayo ilipanga
kusikiliza jambo hili mbali kidogo ikatoa siku 11 sasa, siku 11 pamoja kwamba
tuli-file katika mazingira ya haraka (certificate of urgency) lakini kwa bahati
mbaya haikufanikiwa kusikilizwa mapema kwa hiyo ikatoa nafasi ndefu sana Polisi
kuendelea kunisumbua kuni-harass mimi,wafanyakazi, wanachama na viongozi
wengine wa CHADEMA tunamtaka Mwenyekiti, sasa sikutaka kuonekana Kama
Mwenyekiti Mbowe nakimbia shtaka, siliogopi shtaka kwa sababu ni la
kutengenezeka tu, lakini nilichokuwa nakikataa ni ile kupewa amri na mtu ambae
hana mamlaka kisheria kutoa amri hiyo.
Nataka nchi irejee katika misingi ya
utawala wa Katiba, Sheria na taratibu, Viongozi wa Kiserikali au viongozi wenye
mamlaka juu ya watu wengine wasijione wao wana haki ya kutenda mambo kinyume
cha Katiba, kinyume cha taratibu hata kama jambo wanalotaka kufanya lina njia
njema, lazima yapitie katika mfumo unaokubalika wa kisheria.
Hilo ni jambo la kwanza la msingi sana,
hapa ni Mbowe napambana na dola na pambana na Serikali na pambana na Polisi
napamba na Mkuu wa Mkoa lakini wapo Watanzania wengi tu ambao wanaonewa katika
misingi kama hii na hawana ujasiri wa kupambana na Serikali kuidai haki, kwa
hiyo ninapoidai haki hii sio naidai haki hii, sio kwamba naipigania haki mimi
kama Mbowe hapana, napigania haki katika taifa, taifa liendeshwe kwa mujibu wa
Katiba,Sheria na taratibu za nchi.
Hilo la kwanza lakini la pili Mimi ni
Kiongozi wa watu, ni Kiongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani,Kiongozi wa Upinzani
Bungeni, ni Baba mwenye familia na watoto ni Mbunge wa jimbo la Hai naaminika
na wananchi na mahusiano na taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa,
napokuwa nasikia nimetuhumiwa kwa tuhuma za dawa za kulevya ambazo hazina ushahidi,
haina msingi ni jambo baya sana jambo baya sana ni character assassination.
Nina mipango wa kudai fidia kwa
kuchafuliwa jina, hilo liko wazi nilisema toka siku ya kwanza kwa hiyo mpango
huo lazima tutautekeleza.
Source: Jamii forums media

Post a Comment