DAR ES SALAAM.
Kamishna wa Idara ya Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam, John Msumule ametangaza vita kwa watumishi wa serikali hasa wa uhamiaji wanaohusika na mtandao wa biashara ya utoaji wa vibali bandia vya makazi pamoja na kazi kwa raia wa kigeni.
![]() |
| PHOTO: Kamishna wa Idara ya Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam, John Msumule. |
Ameyasema hayo mapema leo wakati akizungumza na wanahabari, ambapo amesema kuwa idara yake ilifanya ukaguzi kwenye baadhi ya makampuni na kukamata hati za kusafiria ambazo ni bandia zaidi ya 30.
Amezitaja baadhi ya kampuni zilizokutwa na wafanyakazi wenye hati bandia kuwa ni Global Leader, Alpha Romeo Security, na LuckSpin. Aidha, ametoa wito kwa waajiri wote kuhakikisha wana ajiri raia wa kigeni wenye vibali halali vya kazi na makazi, huku akiwataka wageni wasio na vibali kurudi katika nchi walizotoka
Katika hatua nyingine, Msumule amesema ofisi yake imemkamata raia wa Uganda anayefahamika kwa jina la Aisha Talib kwa kosa la kuishi bila kibali nchini, pamoja na kuhodhi pasport 15 za uraia wa Burundi na Madagasca.
Story appeared fistly from mwamba wa habari.

Post a Comment