0
PHOTO: Jenerali mstaafu Michael Flynn.

PIGO KWA RAIS TRUMP.
Mshauri wa Usalama wa taifa nchini Marekani, Jenerali mstaafu Michael Flynn, amejiuzulu jana Jumatatu usiku kufuatia kashfa iliyomkuta ya kuhusiana na mazungumzo aliyofanya na balozi wa Urusi nchini Marekani, Sergey Kislyak, ambayo yalizua utata na mjadala mkubwa nchini Marekani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, Flynn aliwasilisha barua ya kujiuzulu kwa rais Donald Trump jana usiku, ambapo katika barua yake amesema alifanya mawasiliano kadhaa na balozi wa Utusi wakati wa kipindi cha mpito, na kumpa Makamu wa Rais, Mike Pence "habari ambazo hazikukamilika."

Tuhuma zilikuwa zimeibuka kuwa Flynn, ambaye alikuwa kwenye wadhifa huo kwa takriban mwezi mmoja, alizungumza na balozi huyo mnamo mwezi Desemba, kuhusu vikwazo ambavyo Marekani iliiwekea Urusi, licha ya kuwa rais aliyepita Barack Obama bado alikuwa madarakani na kwamba Trump hakuwa ameapishwa kama rais.

Post a Comment

 
Top