Mamlaka
ya Elimu Tanzania (TEA) pamoja na Kampuni ya Sunshine Group Ltd ya nchini China
kwa pamoja zimeingia mkataba wa makubaliano wa miaka mitano ya
kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu katika
mikoa mbalimbali hapa nchini.
DAR
ES SALAAM
Na
John Simon Luhende
Makubaliano
hayo yametiwa saini na kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya
Elimu Tanzania bibi Graceana Shirima na mkurugenzi na mkurugenzi
wa kampuni ya Sunshine Group Ltd bwana Tony Sun Tao leo tarehe 20/2
/2017 katika ofisi za Mamlaka hiyo jijini Dares salaam.
Akizunguza
na waandishi wa habari wakati wa kusainin makubalianao hayo Kaimu mkurugenzi wa
Mamlaka ya Elimu Tanzania bi Graceana Shirima amesema makubalianao
hayo yanawezesha kampuni ya Sun shine kufadhili miradi mbalimbali katika
sector ya Elimu, hivyo basi kupitia makubalianao hayo TEA itakuwa
mratibu mkuu na Sunshine wao watakuwa wakifadhili tu.
Aidha
bi shirima amewashukuru TEA na uongozi wa Sunshine kwa kuona umuhimuwa
kushirikiana katika kutekeleza miradi ya Elimu nchini, na kusemakuwa
katika kutekeleza miradi hii watashirikiana na Wizara pamoja na
Halmashauri.
“Napenda
niwahakikishie kuwa tutaratibu vizuri miradi yote katika muda wote wa
miaka mitano ya makubaliano haya na mamlaka itawatunukia hati ya utambuzi
(CEA) kwa ajili ya kutambua mchango wenu katika sekta hii ya Elimu” alisema
Bi shirima.
Naye
Mkurugenzi wa kammpuni ya Sunshine Goup Ltd Bwana Tony Sun miradi ya
kwanza kutekelezwa kupitia makubaliano hayo kuwa ni ujenzi wa
maabara mbili za sayansi katika shule ya sekondari Matundasi iliyoko
katika Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya na kujengea madarasa na
miundombinu ya Maji katika shule ya Sekondari Bunda iliyopo mkoani Mara na kuongeza kuwa miradi hiyo itagharimu jumla ya apesa za
kitanzania million 210.
“Tutafadhili kwanza katika
mikoa na maeneo ambayo tunafanya shughulizetu katika mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Dodoma, Mbeya,Mara na Mtwara”. Alisema mkurugenzi huyo

Post a Comment