0
Mnada ulifanyika katika jiji la Chesapeake, Maryland uliwakutanisha wauzaji wa vitu kwa njia ya mnada ambapo katka mnada huo bei ya chini kabisa ilikuwa $100,000. Hata hivyo simu iliyotumiwa na Adolf Hitler wakati wa vita kuu ya pili ya Dunia imeuzwa kwa Dollar 243,000 sawa na shilingi za kitanzania 534,600,000 nchini Marelkani.

PHOTO: Aliyezungushiwa duara ni mbwa Alsatian aliyekuwa akimilikiwa na Adolf Hitler ambaye sanamu yake imeuzwa shs 53 milioni.



Maelezo kuhusu mtu aliyeinunua na ambaye aliwasilisha ombi lake la ununuzi kupitia simu, hayajatolewa mpaka sasa, ambapo simu hiyo nyekundu, ambayo imechongwa jina la kiongozi huyo wa Nazi wakati huo, ilipatikana kutoka katika handaki alimokuwa akijificha Hitler wakati huo huko mjini Berlin mnamo mwaka 1945.

Wakati huo wanajeshi wa muungano wa Usovieti waliikabidhi simu hiyo kwa mwanajeshi Mwingereza Sir Ralph Rayner kama zawani muda mfupi baada ya Ujerumani kusalimu amri na kukubali kushindwa katika vita hivyo.
Maafisa wa wapiga mnada hao wanasema simu hiyo ilikuwa kama "silaha ya maangamizi makubwa", kwani ilitumiwa na Hitler kutoa maagizo yaliyopelekea kuuawa kwa watu wengi wakati wa vita hivyo.

Sanamu ya kauri ya mbwa aina ya Alsatian, aliyemilikiwa na Hitler, pia iliuzwa katika mnada huo kwa jumla ya $24,300 ambazo zinakadilia kufika fedha za kitanzania shs 53,460,000 ambapo alinunuliwa na mtu tofauti na aliyenunua simu, mnada huo uliongozwa na wapiga mnada wa Alexander Historical Auctions.

PHOTO: Saa ambayo ilitumiwa na Adolf Hitler kufanya mawasiliano na wafuasi wake kufanya maandamizi makubwa wakati huo.





Source news bbc swahili.

Post a Comment

 
Top