Tamasha linalotoa nafasi kwa wananchi na wanafunzi mbalimbali
kujifunza na kupata fulsa ya kuibua vipaji kuviendeleza, Kufaham Tanzania na
vivutio vyake hasa vilivyo kusini, watoto kupata nafasi ya kujifunza kuchora
katuni na pamoja namaonyesho ya biashara linatarajia kufanyika mkoani Songea hivi karibuni.
![]() |
Muandaaji
mkuu wa Tamasha la Majimaji Selebuka Reinafrida Rwezaura akiongea na wanahabari (hawapo pichani) juu ya tamasha kubwa kwa
mkoa wa Ruvuma.
|
Mshindi wa
pili wa mbio za baiskeli km 100 Allen Nyanginywa (kulia) akiongea juu ya nafasi
aliyopata ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya baiskeli nchini Afrika
kusini katikati ni Reinafrida Rwezaura na kulia ni Muandaaji msaidi wa Tamasha hilo Merania Luoga.
Muandaaji
mkuu wa Tamasha la Majimaji Serebuka Reinafrida Rwezaura akionyesha tiketi tatu za washindi wanaotarajia kuondoka hivi karibuni kuelekea nchini Afrika kusini.
Reinafrida
Rwezaura akimkabidhi tiketi tatu Allen Nyanginywa kwa ajili yake na washindi wenzake wawili (ambao hawakuwepo) ili
kuelekea Afrika kusini kushiriki mashindano.
DAR ES SALAAM.
Tamasha hilo linalojulikana kama MAJIMAJI
SELEBUKA linatarajiwa kufanyika mwaka jana lilifanyika mwaka jana 2016 mwezi wa
Octoba na msimu wa pili kufanyika mwezi Mei 28 hadi 04June 2016 hivyo kupelekea
kufanyika kwa mwaka huu tarehe 23 hadi 30 Julai 2017, ambapo washindi wa mbio
za baiskeli kilomita 100 wanatarajiwa kwenda nchini kushiriki mashindano ya
baiskkeli mwaka 2018.
Akizungumza katika mkutano wa wanahabari muandaaji mkuu wa Tamasha
hilo Reinafrida Rwezaura amesema kuwa “pamoja na nafasi
mbalimbali kama fulsa ya Kupanua soko kwa
wajasiliamali, wafanyabiashara na wanafunzi kupitia midaharo katika shule za
Sekondari kwa wakazi na majirani kwa mkoa wa Ruvuma pia watapata zawadi
kutokana na kushiriki mashindano ya marathoni ya kilomita 42 ambapo mshindi wa
kwanza atapata Tsh 1,500,000, wa pili 1,000,000 na watatu atapata 500,000”.
Vilevile mshindi wa pili wa mashindano ya baiskeli kwa kilomita
100 kutoka mbinga kuelekea Songea Allen Nyanginywa amekabidhiwa tiketi tatu kwa
niaba ya mshindi wa kwanza Salum Miraji na mshindi wa tatu Ipyana Mbogela ambao
hawakuwepo kwa ajilin ya safari ya kuelekea katika mji wa Johannesburg nchini
Afrika kusini kushiriki mashindano ya Chem ride for sight 2017.


Post a Comment