0
Maharusi waliowasisimua watu wengi baada ya kutumia kiasi cha  Sh100 pekee za Kenya kugharimia harusi yao, hivi karibuni waliandaliwa sherehe kubwa ya harusi ambayo imeafanyika hapo jana katikati ya viunga vya jiji la Nairobi.

Haki miliki ya picha AALTONEN JUMBAI
Harusi ya marudio ya Wilson na Anne imeandaliwa katika bustani ya kifahari. 
Sherehe hiyo ya marudio imeandaliwa katika bustani ya Eden Bliss ambayo ni bustani ya kifahari iliyopo viungani mwa Nairobi na imeashimishwa hapo jana wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Wapendanao.
Harusi ya awali ya Anne na Wilson Mutura iligharimu dola moja pekee ya Kimarekani lakini sherehe ya sasa inakadiriwa kwamba imegharimu takribani Ksh 3.5 milioni (zaidi ya Tsh 70milioni).

Pesa hizo zimegharimiwa na makundi mbalimbali yanayohusika katika uandaaji wa sherehe, ambayo yaliungana kwa pamoja na kuchanga pesa kuwaandalia Anne na Wilson sherehe hiyo ya kukata na shoka.
Mmoja wa waandalizi wakuu wa harusi hiyo Aaltonen Jumba kutoka Slique Events Planner Limited, anasema ni vigumu kujua hasa ni kiasi gani cha peza zilitumiwa kuiandaa.
Pamoja na kwamba wahudumu mbalimbali walijitokeza kusaidia kutoa huduma zao, ila hakuna pesa taslimu zilizotolewa. Lakini kuna waliotoa mahema, wengine viti, wengine magari ya kifahari.

Wawili hao wamesafirishwa kwa magari ya kifahari

Kwa sababu walikuwa tayari washafunga ndoa rasmi, kwenye sherehe ya leo, walibadilisha pete zao. Baadhi ya Wakenya mitandaoni wamekuwa wakikosoa uamuzi wa kutumia pesa nyingi kugharimia sherehe nyingine ya harusi kwa wawili hao. L
akini Bw Jumba anasema wanaokosa sherehe hiyo wamekosa kutambua na kufahamu vyema mambo ambayo yamekuwa yakijiri.
"Wawili hao tayari wamesaidiwa kifedha. Wamepewa shamba la kisasa, wakalipiwa fungate na wameahidiwa pesa za kutumia kama mtaji kuanzisha biashara, kwa sababu yote yameshughulikiwa, kwa nini tusiwape kile ambacho walikosa? Kila mtu hutamania sana kuwa na sherehe kubwa ya harusi."

Haki miliki ya picha NDUNGU NYORO / FACEBOOKI
Bw Wilson akisaidiwa kuweka sawa koti lake


Haki miliki ya picha NDUNGU NYORO / FACEBOOK
Bi Anne wakati wa sherehe ya harusi ya marudio

Wawili hao, wanaoishi eneo la Kasarani, Nairobi, walisifiwa kwa kuonyesha thamani halisi ya mapenzi badala ya kuongozwa na pesa.
Zaidi ya kuandaliwa harusi hiyo, wametunukiwa shamba la kilimo cha kisasa, fungate kwenye hoteli ya kifahari na baada ya sherehe ya leo wanatarajiwa kwenda kwa fungate nyingine mjini Dubai.
Dola yenyewe walioyotumia Anne na Wilson katika harusi yao ya mwanzo waliitumia kununua pete mbili. Walikuwa wameahirisha harusi yao mara tatu baada ya kukosa fedha za kutosha kuandaa sherehe kubwa ya harusi. Maombi yao kwa familia na marafiki kuwafanyia mchango, hayakutimizwa.
Baada ya muda, Bwana harusi, Wilson, hakuwa na la kufanya ila kumshawishi mpenzi wake kuhusu uwezo wake. "Wilson aliponieleza hali yake, sikukataa. Mapenzi yetu yalizidi yote," anasema Anne
Ingawa walikuwa na uwezo wa kuishi kwa mtindo wa 'come we stay' uliomaarufu kwa vijana wengi ambapo wapenzi wanaishi pamoja bila kuoana, Wawili hao walikwenda kwa askofu Jasper Owach kutoka Kanisa la Community Christian worship centre mjini Nairobi kurasmisha harusi yao.
"Mapenzi yetu yalidumu kwa muda na ili kujisitiri kutoka maovu baada ya kupata baraka ya wazazi, tuliamua kufanya mambo yetu rasmi," anasema Wilson.

Wilson Muturi na mkewe Ann walitumia dola moja pekee wakati wa harusi yao

Siku yenyewe ilipofika, bwana Harusi, Wilson aliwashangaza waumini baada ya kukimbia nje sherehe ikiendelea. 
"Alitoka ghafla kununua pete ya harusi nilipokuwa naendelea na shughuli ya kuwafunganisha," alisema askofu Jasper Owach, ambaye aliongoza hafla hiyo.
Wilson alirejea na walipokuwa wanatamka kauli za ndoa, Wilson alitoa pete hizo zilizofungwa kwa gazeti na wakavikana pete. Wawili hao, wamewapa hamasa vijana kutozuiwa na uwezo wao wa kifedha na hivyo basi kuhalalisha mapenzi yao kupitia ndoa.






This story is from & appeared firstly on bbcswahili.

Post a Comment

 
Top