Takribani watanzania wapatao 132 wanaoishi nchini
Msumbiji wamefukuzwa nchini humo huku wengine wasiojulikana wakidaiwa kukamatwa
kufuatia operesheni iliyoanzishwa na serikali ya nchi hiyo hivi karibuni.
![]() |
| Sehemu ya mji Monte Puez nchini Msumbuji ambao ni maarufu kwa uchimaji wa madini. |
Kulingana na taarifa ya serikali ya Msumbiji inasema operesheni
hiyo inalenga kuwatimua raia wa kigeni wanaoishi nchini humo kinyume cha
sheria.
Kwa upande wa taarifa ya
wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki nchini Tanzania
imesema kuwa raia waliofukuzwa ama kukamatwa ni wale wanaoishi mji wa Monte
Puez kwa kuwa una raia wengi wa kigeni ikilinganishwa na miji mingine.
Kutokana na taarifa hiyo
tayari ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji unaendelea kufanya mawasiliano ya
kidiplomasia na serikali ya Msumbiji ili kuwahakikishia usalama raia wa Tanzania
na mali yao nchini humo upo salama
Inakadiriwa kuwa, Watanzania wapatao
elfu tatu (3,000) wanaishi na kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii katika
mji huo wa Monte Puez, ambapo hatua hiyo inakuja licha ya mataifa ya Msumbiji
na Tanzania kufanya mkutano wa kuainisha maeneo ya ushirikiano yakiwemo maswala
ya kibiashara na uhamiaji.
Huku operesheni hiyo ikiendelea hivi
karibuni serikali imekuwakumbusha Watanzania wote waishio ughaibuni, kufuata
Sheria na taratibu za nchi hizo wanazoishi ili kuepukana na madhara yoyote
yanayoweza kujitokeza pindi wananapokuwepo katika nchi hizo.
Firstly appeared in bbcswahili.

Post a Comment