Kila
raia ana tashwishwi ya kupata haki pale panapokuwepo na hitaji litokanalo na
uwepo wa sheria pindi sheria inapovunjwa au kupindishwa kutokana na makossa
ikiwa na maana pasipo makosa basi hakuhitajiki sheria maana itakuwa butu pasi kutumika.
![]() |
Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya
Arusha Sekera Mosho akitoa hotuba wakati wa maadhimisho hayo mapema leo jijini
Arusha.
|
![]() |
Meya wa jiji la Arusha Lazaro Karisti
kushoto akiteta jambo na Jaji mstaafu (….) kulia na wengine ni majaji wa mahakama kuu wakati wakielekea katika
viwanja vya maadhimisho ya siku ya Sheria.
|
![]() |
Mahakimu na wanasheria wa mkoa wa Arusha wakiwa katika maandamano kuelekea eneo la sherehe ya siku ya Sheria nchini.
|
ARUSHA.
Wanasheria
nchini wameadhimisha siku ya sheria ikiwa ikiwa a kauli mbiu “Umuhimu wa utoaji haki kwa wakati
kuwezesha ukuaji wa uchumi” ambapo mkoan Arusha sherehe hizo zimefanyika
katika viwanja vya mahakama kuu ya kanda ya Arusha na kuhudhuliwa na viongozi
mbalimbali.
Akitoa
hotuba ya chama cha mawakili Tanganyika kanda Arusha, Mwenyekiti wa chama cha
mawakili wa kujitegemea kanda ya Arusha Modest Akida amesema, maudhui ya kauli
mbiu ya mwaka huu yamelenga kwenye msukumo wa serikali ya awamu ya tana wa
kujenga uchumi, ikiwa na maana pamoja na mambo mengine, biashara na uwekezaji.
“ukuaji wa biashara na
ongezeko la uwekezaji huenda sambamba na mfumo wa utoaji haki katika nchi
ambapo kazi kuu ya mfumo huo ni kulinda haki pale migogoro inapotokea” alisema Modest Akida, Mwenyekiti wa mawakili wa kujitegenmea.
Wakati
haki ni neno lililozoeleka midomoni pamoja na masikioni mwa watanzania, wakati
huo huo kila uchao watoto, vijana, wanawake, wanaume, wazee, kina mama,
wafanyakazi, waajili kwa ujumla siku haipiti miongomi mwao kusikia wakidai
haki. Neno hilo ‘haki’ ni dhana pana inayohusisha mamlaka mtambuka.





Post a Comment