Kama umekuwa mbali na habari ya siku ya sheria nchini basi nakuletea tukio la kipekee tunavyoweza kusema pia kupitia captured photos baadhi ili uweze kupata habari hii.
| Bango lenye ujumbe ambalo huyo mama alikuwa kalibeba ili kufikisha ujumbe. |
| Akisukumwa na afisa usalama (mwenye koti jeusi) ili aondoke eneo la mbele alipokuwa huyo mama aliyenyosha mkono. |
| Mara baada ya Rais kupata taarifa na kuona tukio lile aliruhusu aende mbele na kupata nafasi ya kuelezea kwa undani kisa na mkasa wa yeye kwenda pale. |
| Rais Magufuri kulia na Jaji mkuu kushoto wakimsikiliza mama alipokuwa anatoa maelezo kuhusu alichodai dhuruma anayofanyiwa kuhusu mirathi. |
| Akitoa maelezo kwa kina huku akigusia na baadhi ya vitisho vya kuuwawa. |
DAR ES SALAAM.
Kwa upande mwingine kutoka jijini Dar Es Salaam katika maadhimisho hayo ya siku ya Sheria nchini mama mmoja ambaye aliibuka gafla akiwa na bango lenye kuwaraumu baadhi ya viongozi wa serikali, wanasheria, mahakimu, mwendesha mashitaka wa serikali na jeshi la polisi kwa kutosimamia kesi yake inayohusu mirathi.
Wakati msimamizi wa sherehe akitangaza hatua ya upigaji wa picha mama huyo anayesemwa kuwa jasiri kutokana na kitendo hicho alionekana na wanausalama ambapo mmoja alimzuia na kuanza kumsukuma huku akizuia lile bango lenye ujumbe lisionekane kwa Rais, lakini kutokana na mazingira hayo Mh. Rais aliona tukio lile na kuomba yule mama aachiwe na kwenda kumueleza undani wa madai yake.
Kufuatia hali hiyo mara baada ya kupata nafasi ya kuelezea madai yake na Rais Magufuri kumsikiliza aliamuru mama huyo apewe ulinzi kutokana na mazingira ambayo yanaweza kuleta sintofahamu ambayo yanatokana na taarifa za yeye kutaka kuuwawa na watu waliomtumia ujumbe.
UPDATES ZAIDI HAPA HAPA >>>
Post a Comment