Vyuo
Vikuu hapa Nchini vimeagizwa kuacha mara moja kutoza ada kwa fedha za kigeni
kwa wanafunzi ambao ni watanzania, vinginevyo hatua kali za kisheria zitatumika
kwa yeyote atakayepatikana akitoza ada kwa fedha hizo.
![]() |
| Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia mhandisi Stella Manyanya. |
KUTOKA DODOMA.
Agizo
hilo limetolewa jana Bungeni mjini Dodoma na naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia mhandisi Stella Manyanya alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge
Jaku Hashimu Ayoub kuwa kumekuwa na malalamiko ya wanafunzi wa Elimu ya Juu
Tanzania ambao ni wazawa kulipishwa ada ya masomo kwa fedha za kigeni badala ya
fedha za Kitanzania.
“Sarafu inayotakiwa
kutumika Tanzania ni shilingi ya Kitanzania kwa mujibu wa kifungu cha 25 na 26
cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ya mwaka 2006. Aidha, kwa Tanzania
malipo ya kitu au huduma yoyote inapaswa kulipwa kwa shilingi ya Kitanzania
kama ilivyoainishwa kwenye kifungu cha 28 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania
2006” alifafanua Mhandisi Manyanya.
Aliendelea
kwa kusema kuwa mpaka sasa wizara haijapokea malalamiko yoyote ya kutozwa fedha
za kigeni kwa wanafunzi wa elimu ya juu tangu itoe agizo kama hilo kwa wamiliki
wa vyuo Septemba 07, 2016.
Ikiwa
ni kwa mara nyingine Mhandisi Manyanya ameviagiza vyuo ambavyo bado vinatoza
wanafunzi Watanzania fedha za kigeni kuacha mara moja kwani vyuo hivyo
vimeelekezwa kutoza wananchi wa Kitanzania kwa pesa ya Kitanzania.
Aidha
Mhandisi Manyanya amewataka watanzania kutoa taarifa Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia ikiwa kuna Chuo chochote kinachotoza ada kwa
Watanzania kwa fedha za Kigeni ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe dhidi
ya wahusika.
![]() |
Waziri wa fedha na mipango Philip
Mpango.
|
Wakati
huohuo Waziri wa Fedha na Mipango Philip
Mpango alitoa onyo kwa shule zinazotoza ada kwa fedha za kigeni kuchukuliwa
hatua kali za kisheria ambapo alisema, ikiwa kuna mwananchi yeyote anayetozwa
ada kwa fedha za kigeni basi atoe taarifa mapema ili hatua stahiki zichukuliwe
kwa wahusika..


Post a Comment