![]() |
Nchi ya somalia inaendelea kukumbwa na
mashambulizi ya kujitoa mhanga na yale yanayoendeshwa kwa kutumia magari
yaliyotegwa mabomu.
|
MADINA -MOGADISHU.
Zaidi ya watu 30 wameuawa na wengine 50 kujeruhiwa
katika mlipuko wa bomu lililotegwa ndani ya gari katika mtaa wa Madina mjini
Mogadishu nchini Somalia, watu waliofanya shambulio hilo walitumia gari ambalo
lilikuwa na vilipuzi na kugharimu maisha ya watu zaidi ya watu 30 katika mtaa
wa Madina kusini mwa Somalia, kwa mujibu wa idara za usalama nchini Somalia.
Shambulio hili ni la kwanza kufanyika kipindi kifupi
baada ya kufanyika kwa uchaguzi na katika utawala mpya wa Rais wa Mohamed
Abdullahi Farmajo Mohamed ambaye alichukua hatamu ya uongozi baada ya kuteuliwa
na Wabunge na Maseneta wa nchi hiyo.
Jumamosi ya juzi ofisa mwandamizi wa kundi la Al
Shabab alitangaza kuwa watafanya shambulizi kulenga wafuasi wa rais huyo mpya
wakidai kuwa anaendeshwana mataifa ya magharibi, hata hivyo mpaka sasa hakuna
kundi lolote ambalo limekiri kuhusiana na tukio hilo, hata kama kundi la Al
Shabaab linanyooshewa kidole.
![]() |
| Milipuko imekuwa ikiendelea pamoja na mashambulizi ya kujitoa mhanga na yale yanayoendeshwa vikundi vya kigaidi na kwa kutumia magari yanayotegwa mabomu. |


Post a Comment