Dar
Es Salaam, Baada ya wanandoa ambao ni wanamuziki
maarufu wa nyimbo za Injili, kuingia katika mzozo miaka minne iliyopita, mmoja
wao Flora Mbasha amechumbiwa na anatarajiwa kufunga ndoa ya pili hivi karibuni
mkoani Mwanza.
![]() |
PROFILE PHOTO:
Wedding
portrait picture.
|
Sakata hilo linaweza
kuibua mjadala miongoni mwa waumini wa dini ya Kikristo ambayo pamoja na
kuruhusu ndoa kuvunjika, ni nadra sana kwa makanisa kuidhinisha suala hilo.
Habari za kuaminika
ambazo Mananchi Digital imezipata zinasema vikao vya maandalizi ya harusi hiyo
vimeshaanza baada ya Flora kufanikiwa kupata talaka aliyoidai Mahakama ya
Wilaya ya Kinondoni jijini hapa.
Flora, ambaye ni mjukuu
wa aliyekuwa muhubiri maarufu nchini, Askofu, Moses Kulola (sasa marehemu),
tayari amevishwa pete ya uchumba na amebadili jina la kisanii akitaka mashabiki
wake wamtambue kama “Madame Flora” badala ya jina aliloibukia la Flora Mbasha.
Asili ya neno “madame”
analotumia Flora ni Ufaransa na linamaanisha mwanamke aliyeolewa.“Kwa sasa siwezi kukwambia chochote kuhusu hilo. Sijui, labda
ifikapo Machi naweza kuzungumza,” amesema Flora, ambaye alitamba na kibao cha
“Jipe Moyo”.
![]() |
PHOTO: Frola Mbasha ambaye kwa sasa anataka kutambulika kama
Madame Frola.
|
habari hii imetoka @mwananchi digital


Post a Comment