0
PHOTO PROFILE: Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza. 

ARUSHA.
Serikali ya Burundi imetoa tamko jana Jumatano kwamba haitapeleka ujumbe wake katika mazungumzo ya upatanisho yanayoendelea  jijini Arusha, Tanzania.


Mazungumzo hayo yanayolenga juu ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa nchini Burundi yalitarajiwa kuanza leo Alhamisi, lakini kuna wasiwasi ulioendelea kwamba mazungumzo hayo hayatasaidia kuleta amani katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati inayokabiliwa na mgogoro wa kisiasa.

Wapinzani na asasi za kiraia wanasema msimamizi wa mazungumzo hayo, rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa, anavuruga mchakato huo kwa kuwakaribisha wanasiasa ambao walifanya jaribio la kumpindua Rais Pierre Nkurunziza mwaka 2015.






Appeared first in VOA Swahili.

Post a Comment

 
Top