0
Harakati anazozifanya mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda  huku akiungwa mkono na viongozi wa kada mbalimbali wakiwepo wa dini, zimekuwa zikishika kasi kwa mataifa jirani na  miji mikubwa kama Harare, Kampala, Kigali, Mombasa, Nairobi nk kote huko ni Makonda, Magufuri na Tanzania.

Kamanda Charles Mkumbo akionyesha mihadarati aina ya mirungi.

Kamanda Charles Mkumbo akionyesha mihadarati aina ya mirungi kwa wanahabari

Kamanda Mkumbo akionyesha madawa ya kulevya aina ya heroin kwa wanahabari

ARUSHA.
Wakati nchi ikiwa kwenye mchakamchaka wa utafutaji, kuwakamata, watumiaji, wauzaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya, ambapo wamekuwa wakijihusisha na madawa hayo haramu ambayo yamekuwa yakiharibu kwa kiasi kikubwa jamii nchini.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha kamishna Charles Mkumbo amekutana na wanahabari na kuwaonyesha madawa kadhaa yaliyokamatwa mkoani humo ikiwa ni katika mkakati unaoendelea nchini kote kutokomeza madawa hayo.


Akionyesha kwa waandishi wa habari baadhi ya madawa ya kulevya yaliyo kamatwa aina ya mirungi pamoja na bangi ambapo wamefanikiwa kuyakamata madawa ya kulevya aina ya bangi misokoto 3845 kete 167 za.madawa ya kulevya aina ya heroin.


Post a Comment

 
Top