0
PHOTO PROFILE: Agnesy Gerald alimaarufu Masogange.


Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro ametoa taarifa ya kupelekwa kwa Mkemia mkuu wa Serikali kwa ajili ya kupimwa na kuchukuliwa vipimo vya damu ili kubaini kama anatumia dawa za kulevya mtuhumiwa Agness Gerald.


Mtuhumiwa huyo ambaye anafahamika kwa jina maarufu la Masogange ambaye pia ni mrembo maarufu anayetamba katika video za wasanii mbalimbali wa bongo fleva alikamatwa na polisi juzi.

Kamishna Sirro amewaambia wanahabari leo kuwa Masogange amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kwamba majibu yakipatikana kesho atafikishwa mahakamani

"Tunamchunguza Masogange katika mambo matatu ili kujua kama anauza , anatumia au anasafirisha dawa za kulevya, " amesema Kamishna Sirro.

Katika hatua nyingine, Kamishna Sirro amesema watuhumiwa 349 wamekamatwa kwenye operesheni ya kupambana na dawa za kulevya iliyoanza Februari Mosi mwaka huu.







Chanzo: Muungwana

Post a Comment

 
Top