Chama cha wananchi CUF kikiwa katika msuguano wa kiuongozi na Prof. Ibrahim
Lipumba kutokana na msigano wa kiuongozi, chama hicho leo kupitia mkutano mkuu
wa tawi la Chanjaani, Jimbo la mkoani wilaya ya Mkoani-Pemba kimefanya maamuzi
ya kumfukuza uanachama wa CUF ili aweze kuendelea na majukumu yake mtaani Mohamed Habibu Mnyaa.
![]() |
| Profile PHOTO: Mohamed Habibu Mnyaa. |
MKOANI PEMBA.
Fukuza hiyo imetokana na Mohamed Mnyaa kwenda kinyume na kukiuka katiba ya
chama hicho kwenye Ibara ya 12 (6)(7)(16) ambapo inasemekana amekuwa na mienend
isiyofaa inayopelekea kuwagawa wanachama, kueneza taarifa za upotoshaji dhidi
ya viongozi na Chama, pia vitendo vya hujuma za kutaka kukidhoofisha Chama, kudharau
na kushindwa kuhudhuria pamoja na kushinwa kutoa ushirikiano kwa tawi lake pale
alipotakiwa kufanya hivyo.
Akitoa maamuzi hayo katibu wa tawi
la Chaanjani jimbo la mkpani Pemba Kombo mohamed maalim amesema mkutano wetu mkuu wa leo umehudhuriwa na wajumbe halali 112 kati
ya wajumbe wote halali 113, hivyo wajumbe wote 112 wamepiga kura za ndio
kuazimia kumfukuza uanachama kwa mujibu na mamlaka ya kikatiba yaliyoelezwa
katika katiba ya CUF uliopo ukurasa wa 29 ibara ya 18 kifungu (1)(ix) kuhusu wajibu
wa mkutano Mkuu wa Tawi kama ilivyoeleza;
“Kumchukulia hatua za nidhamu mwanachama au
kiongozi yeyote wa tawi, ikiwa ni pamoja na kumpa onyo, karipio, karipio
kali, kumsimamisha uanachama au uongozi wa Chama kwa muda, na hata kumuachisha
au kumfukuza uanachama wa Chama”
Mohamed
Habibu Mnyaa ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo la Mkanyageni kwa vipindi
viwili 2005 mpaka 2015 alijiunga na CUF katika tawi hilo tarehe 28 septemba
mwaka 1999 ambapo alikabidhiwa kadi yenye namba 029033. Maalim ameongeza kuwa mwenendo
huo mbaya na usiofaa kwa Chama na viongozi wake tangu alipokosa ridhaa ya
wanachama na Maamuzi ya vikao vya Chama kumpitisha kugombea kwa mara nyingine
tena katika nafasi ya ubunge mwezi August, mwaka 2015.
Maalim alisema “Tunatoa wito kwa wanachama wote wa tawi la Chanjaani,
kuzingatia wajibu wao wa kikatiba na kuheshimu taratibu, kanuni na kulinda
nidhamu na heshima ya Chama chetu ndani ya Chama na ndani ya jamii kwa ujumla.
Uongozi wa tawi hautasita kutekeleza matakwa ya katiba pale itakapobainika kwa
mwanachama yeyote kwenda kinyume na maamuzi na misimamo ya Chama”
Kombo mohamed maalim
Katibu wa tawi la chanjaani,
jimbo la mkoani-pemba Imetolewa
leo Tarehe 7/2/2017

Post a Comment