0
Mkutano wa wadau wa madini mkoa wa Arusha umewakutanisha wafanyabiashara na wachimbaji wadogowadogo akiwemo mchimbaji mkubwa wa Tanzanite One nchini  ili kuangalia sababu ya uhaba wa madini ya Tanzanite ambayo yanachimbwa na kupatikana Afrika nchini Tanzania tu pekee.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akiongea wakati mkutano wa wadau wa madini wakiwemo wafanyabiashara, wauzaji watafuta wateja na uongozi wa wao jijini Arusha leo.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo, katikati, Faizal Juma Shahbhai –Mkurugenzi Tanzanite One na kulia ni kushoto ni mwenyekiti wa wachimhaji, na brokers wakisikiliza maoni na maombi ya wafanyabiashara na wachimbaji wadogo wa madini, (hawapo pichani)
Wauzaji, watafutaji, wachimbaji wadogowadogo wa majini jijini Arusha wakiwa makini kumsikiliza Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (hayupo pichani) alipokuwa akiongea nao juu ya matatizo yanatowasibu.






ARUSHA.
Katika mkutano huo unaoegemea kutatua kero mbalibali zikiwepo za uhaba huo wa madini na kuepusha uhaba wa fedha kwa wadau hao kutokana na madini mengi kuchimbwa na kusafilishwa nje ya nchi, pamoja na kukosekana kwa mapato yanayoweza kuwasaidia wao na familia zao.

Kufanyika kwa mkutano huo ambao ni muendelezo wa mikutano, vikao vingi vilivyowahi kufanyika hapo nyuma ili kuangali namna ya kutatua matatizo mengi yanayojikita katika uchimbaji wa madini ususani mkoani Arusha.

Akiongea wakati wa mkutano na wadau mbalimbali, mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo amesema pamoja na kuwepo kwa  shida ya upatikanaji wa eneo kufanyia biashara ili kutatua mazingira ya kufanya biashara, kumekuwepo na baadhi ya viongozi wa wachimbaji na wauzajiwasiokuwa na elimu ya kulipa mkodi, wengi wamekuwa wanakimbia kulipa kodi kutokana na kutokuwa na elimu ya ulipajiwa kodi.


“mfano vijana wa bodaboda wao mapato yao hayafiki zaidi ya milioni 4 kwa mwaka hivyo hawalipi kodi ila wanatakiwa kupeleka taarifa ya mapato yao kila mwaka TRA ili kuweka kumbukumbu, mnajua Tanzania ndiyo nchi pekee ambapo madini haya yanapatikana hivyo kuna umuhimu wa wananchi nao kupata manufaa, hata hivyo hapo nyuma mlionekana kuwa deal kwa askali lakini kwa sasa limepungua” amesema Gambo.

Katika hatua nyingine Kampuni inayomiliki mgodi wa Tanzanite One ambao hapo kabla umekuwa ukilalamikiwa na wadau hao kwa kutowashirikisha katika hatua na mabadiriko wanayofanya juu ya kuwapatia mabaki wananchi ili kuweza kupata nafasi ya kuchmbua na kupata masalia ya Tanzanite imeweza kuwakumbusha Watanzania na hasa wananchi kuhusu masalia hayo.

Mkurugenzi wa TANZANITE ONE Faisal Juma Shahbhai amesema kuwa, "kwa miaka miwili tu tumejitahidi kulipa madeni yanayodaiwa na makampuni mbalimbali ikiwepo NSSF na mengine wengi, katika kufanya hivyo tulipoteza ule uharisia wa mwanzo wa kuweza kuwasaidia wananchi".


Kampuni ya Tanzanite One ambayo hapo kabla ilikuwa chini wa wamiliki wengine kutoka Afrika kusini iliuzwa na kununuliwa kwa mzawa ambapo kabla ya kuuzwa mwaka 2014 iliacha madeni yaliyokadilia kufikia shs 30bilioni ambapo chini ya uongozi mahiri wa Faisal wameweza kulipa madeni yote ndani ya miaka miwili tangu waliponunua kampuni hiyo ianyozalisha madini yanayopatikana nchuni Tanzania tu katika Afrika.

Ameongeza kwa kusema kuwa “mimi ni mdau na mmiliki katika mgodi huo ila kutokana na sheria mbalimbali zilizopo na nilizozikuta ni ngumu kuzibadilisha kwa sababu hiyo ni vema kuwa na uvumilivu maana ni kama mtu aliyefunga ndoa na kampuni hivyo ni vigumu kufanya yale uliyokuwa unafanya huko nyuma ndani ya ndioa uliyopo , kama mimi wakati nikiwa broker"

Faizal Juma Shahbhai –Mkurugenzi TANZANITE ONE.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo wa Tanzanite One Faisal aliwasaidia wachimbaji hao kwa kuwapa shs 10 milioni kwa ajili ya kuanzishia mfuko maalum wa wachimbaji hao.



Post a Comment

 
Top